Wafanyabiashara wa chakula mjini Kasulu mkoani Kigoma
wametakiwa kusafisha mazingira yanayo wazunguka kwa kuweka maji tililika kwa ajili
ya usafi wa mikono ili kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Agizo hilo limetolewa na afisa afya na mazingira wa halmashauri
ya Mji wa Kasulu Bw Msafiri Charles wakati wa mahojiano na Buha News ofisini
kwake kuhusu kampeni ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa April mosi mjini
Kasulu.
Amesema ni wajibu wa kila mjasiliamali wa chakula
kufanya biashara kwa kuzingatia ubora wa afya kwa mteja wake.
Ameeleza kuwa baadhi ya wajasiriamali wanafanya
biashara bila kuweka vifaa sahihi vya kusafishia mikono na wengine kusogeza
biashara za chakula karibu na dampo la uchafu bila kujali madhara yatakayo
jitokeza.
Amebainisha kuwa athari za uchafu ni pamoja na
magonjwa ya mlipuko ikiwemo na kipindu pindu na homa za mtumbo yanayo pelekea upotevu
wa maji mwilini
Sambamba na hilo Bw. Msafiri ameelekeza uongozi wa kila
kata kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wasio kuwa na vifaa vya
kutunzia uchafu na wanao fanya biashara
sehemu hatarishi.
Kwa upande wake Happiness Nkone ambaye ni mjasiliamali
mkongwe wa chakula eneo la Mnadani amekiri kuwepo kwa mulipuko wa magonjwa yanayotokana
na kula chakula kichafu
“Tunashindwa kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya
usafi sio kwamba atujui apana lakini ni mtaji mdogo hivyo kulazimika wateja
wetu kunawa kwenye chombo kimoja” amesema Happiness
0 Comments