Marais kutoka nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa
Afrika na jumuiya ya Afrika mashariki wameipongeza Tanzania kwa kuwa na
muungano wa kipekee duniani ulioziunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Burundi Sylvestre
Ndayishimiye Pamoja na Rais wa Comoro Azali Assoumane wakati wa sherehe za kilele
cha maadhimisho ya siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika
Jijini Dar es Salaam
Marais hao kwa Pamoja wakiwawakilisha wengine
wameishukuru Tanzania kwa mchango mkubwa iliyoutoa wakati wa harakati za
kupigania uhuru wa mataifa yao Pamoja na ushirikiano wa kiuchumi unaoendelea
baina ya nchi za SADC na Afrika kwa ujumla.
Akihutubia watanzania na wakazi wa afrika mashariki
Rais Ndayishimiye amebainisha kuwa Tanzania imekuwa na mchango mkubwa kwa
maendeleo ya nchi ya Burundi na nyingine
Ndayishimiye amesisitiza kuwa pamoja na kuwa Jirani wa
nchi nyingi watu wake wana unasaba na nchi za Burundi, Kenya Uganda, Comoro,
Zambia, Malawi na Zimbabwe na kusisitiza kuwa husezi kuwatofautisha kwa namna
yoyote ikiwemo lugha na mahusiano ya kiutamaduni
Kwa upende wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. Samia Suluhu Hassan amehimiza watanzania kudumisha umoja wao ambao
unaunganishwa na lugha ya Kiswahili sambamba na kuendeleza shughuli za
maendeleo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesherehekea miaka 60
ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Marais wa kwanza wa nchi hizo
hayati Julius Nyerere na Abeid Amani Karume
0 Comments