Zaidi ya shilingi Bilioni 15 zimetolewa na serikali kuu kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kager ana kuchangia ukuaji wa sekta
mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Hayo yamebainishwa jana na Mbunge
wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Adv Stephen Byabato wakati akihutubia mkutano wa hadhara na
wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini ambao umefanyika katika viwanja vya
Soko
kuu la Manispaa
hiyo.
Mhe. Byabato amesema kuwa katika miaka 3
ya Rais Dr. Samia Suluhu
Hassan ambayo
inahitimishwa mwezi huu
serikali ya awamu ya 6 imetoa
fedha nyingi ambazo zilisaidia kuboresha mindomibinu ya elimu, Barabara, huduma
za afya na Uchumi kwa wakazi wa Jimbo la Bukoba mjini
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa mbunge Stephen Byabato mjini Bukoba
Amesema kuwa kupitia fedha hizo baadhi ya maeneo ambayo hayakuwa na shule yamepata huduma hiyo kwa kujengewa shule mpya za msingi na sekondari sambamba na kuanzisha huduma za Viwanda, Biashara na uwekezaji.Miradi mingine ya mafanikio ni pamoja na uwekaji wa taa za Barabarani, Marekebisho katika Soko kuu, Usafishaji wa mto Kanoni, Ujenzi wa Hospitali ya wilaya iliyopo Nshambya pamoja na uunganishaji umeme kwa wananchi kupitia miradi inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini - REA.
Kufuatia kuwepo kwa mafanikio hayo sambamba na uwepo wa mahitaji mengine ya maendele, Mheshimiwa Byabato ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.
Pamoja na mambo mengine Mh. Byabato amejindua mashindano ya mpora wa miguu katika jimbo hilo kwa kukabidhi jezi, mipira pamoja na pesa tasilimu kiasi cha sh. 200,000 kwa kila kata kwa ajili ya maandalizi ya Jimbo Cup
Marchi 19 mwaka huu Rais Dr. Samia Suluhu Hassan
atatimiza miaka mitatu tangu alipoapishwa kuwa Rais kufuatia kifo cha alitekuwa
rais wa jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli
Mwandishi: Mariam Kagenda
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments