Mkuu wa mkoa wa Kigoma ahimiza jamii kuenzi muungano

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuuenzi, kuulinda, kuimarisha, kuudumisha na kukuza ushirikiano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar kwaajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote mbili zote mbili 

Mh. Andengenye ametoa rai hiyo leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kimkoa yamefanyikia katika viwanja vya CCM Umoja mjini Kasulu

Amesisitiza kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa na manufaa makubwa na kwamba kila mtanzania hana budi kuuenzi kwa kushiriki shughuli za maendeleo 

“Tuendelee kulinda muungano wetu kwa misingi imara tuliyoikuta kwa kudumisha amani, kuendeleza mshikamano,umoja na utulivu ili rasilimali zetu, maliasiri  na vivutuo mbalimbali tulivyopewa na Mwenyezi Mungu, viendelee kutoa fursa zinazoweza kuleta maisha bora zaidi kwa kila mtanzania.  Sote tukitimiza wajibu wetu, nafasi ya kusonga mbele kimaendeleo itaendelea kuimarika na kuwa kubwa zaidi” Amesema Andengenye.


Ameongeza kuwa kwa kuthamini juhudi za waasisi wa muungano, na mafanikio yaliyopatikana kwa pamoja tuendelee kuthamin, kuudumisha na kuulinda muungano wetu muungano ambao ni adimu na adhimu.


ametaja mafanikio yaliyotokana na serikali ya muungano kuwa ni pamoja na kuimarisha huduma za jamii, amani na utulivu.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viomgozi mbalimbali kutoka wilaya zote za mkoa wa Kigoma, viongozi wa vyama vya siasa, wafanyabiashara pamoja na wananchi 


Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments