Akihutubia
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika jana katika ukumbu wa Chuo cha
Ualimu Kasulu, Prof. Ndalichako amebainisha kuwa, ametoa ufadhili huo baada ya
kupata na kusoma mwongozo wa Chama cha mapinduzi wa kuimaridha mashina kuelekea
uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Amebainisha kuwa
viongozi wa mashina wamepewa kipaumbele katika mwongozo mpya wa Chama ili kuhakikisha
muundo wa uongozi na usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi unakuwa
shirikishi.
“Nilitembelea
makao makuu ya chama na kukabidhiwa mwongozo huu unaoonesha wajibu wa viongozi
wa shina katika uchaguzi na usimamizi wa shughuli za maendeleo, baada ya
kuusoma nilibaini kuwa njia kuu ya kuwawezesha mabalozi kutekeleza wajibu wao
huo ni kuwapa mafunzo, na ndiyo maana nimetoa ufadhili huu ili mjengewe uwezo
kwa kujua wajibu wenu na pia mfahamu nini ni dira ya Chama kuelekea chaguzi
zijazo” alisisitiza Prof. Ndalichako
Profesa
Ndalichako amebainisha kuwa viongozi wa chama ngazi ya shin ani msingi imara wa
kusimamia na kulinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali huku akimpongeza
Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya
maendeleo katika ngazi za mitaa na vijiji ambako viongozi wa Shina wanatoka
“Nikitafakari
nilipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo miaka takribani minne iliyopita hali
ilivyokuwa na hatua tuliyofikia kwa sasa, sina budi kumshukuru mheshimiwa Rais Samia
kwa kutoa mamilioni ya pesa katika jimbo hili, ninyi mabalozi ni mashuhuda,
tumeupiga mwingi na harakati za kuleta maendeleo zaidi zinaendelea”
alisisitiza Mh. Prof. Ndalichako huku akishangiliwa na viongozi hao
Pamoja na mambo
mengine Profesha Ndalichako amegawa Bendera 550 za chama cha mapinduzi zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya mashina yote ndani ya
jimbo hilo kwa lengo la kuonesha uhai wa chama katika ngazi za ubalozi.
Akihutubia katika uzinduzi wa mafunzo hayo katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Bw. Mobutu Malima aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, amepongeza uamuzi wa mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako wa kufadhili mafunzo kwa viongozi wa mashina akitaja kuwa chama msingi wake ni Shina.
Bw. Malima amekiri
kuwa kitendo cha kuwakusanya mabalozi katika mafunzo hayo ni cha thamani kubwa
na kinapaswa kupongezwa, huku akiwahimiza mabalozi kuutambua umhimu wao
“Mabalozi
ndio viongozi wakuu wa Chama ngazi ya shina, ndio wenye mamlaka kamili ya
kusajili wanachama wapya na kusimamia mienendo ya wanachama, na endapo
mwanachama anakiuka miiko a maadili ya chama mabalozi ndiyo wanaotambua na
kumpa mwanya mwenyekiti wa CCM taifa kuchukua hatua, kwa maana hiyo viongozi
wakuu wa chama ni wawili yaani mwenyekiti wa shinda na mwenyekiti wa taifa,
lazima tuwaheshimu na tuwajengee uwezo ili watimize wajibu wao ipasavyo”
Alisisitiza katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Mobutu Malima
Bw. Malima amewataka
viongozi wote wa kuchaguliwa kuendelea kuwatambua viongozi wa shina na kuwapa
ushirikiano ili kukijenga chama na kukipatia ushindi katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka huu
“Profesa Ndalichako
nakupongeza sana kwa namna unavyofanya kazi za kibunge na kuimarisha chama,
hakika ningekuwa mpiga kura wa Jimbo hili ningekupigia kura, bahati mbaya mie
si mpiga kura wako lakini ninaamini utashinda, na niseme tu kitendo hiki cha
kuwakutanisha mabalozi umewachiongea na wabunge wengine, nitaandaa walaka kutoa
maelekezo kila jimbo lifanye jambo kama hili” Aliweka bayana ndugu Malima.
Hii ni Mara ya
kwanza kwa viongozi wa CCM ngazi ya shinda kukutana kwa Pamoja katika ngazi ya
jimbo tangu kuasisiwa kwa Chama cha mapunduzi mwaka 1977.
MATUKIO KATIKA PICHA
Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akionesha msisimko wa kipekee wakati akishuhudia shamrashamra za mabalozi waliokuwa ukumbini tayari kupokea maelekezo ya Chama. Kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Mobutu Malima
Katibu tawala wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele akiwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kigoma Bi. Agripina Zaituni Buyogera baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo kwa mabalozi mjini Kasulu
0 Comments