Si jambo geni kwamba katika siku
za hivi karibuni, harakati mbalimbali za kisanii nchini Tanzania zimekuwa
mstari wa mbele katika kuibua upya vipaji vya vijana. Venice na maonesho ya kimataifa ya sanaa ya kila baada ya miaka miwili,
kwa kuzingatia umakini mkubwa uliotolewa kwa Afrika katika Maonesho ya mwaka
2022, kwa hakika ni mwanzo kwa "upepo huu wa kisanii" unaovuma kutoka
katika Bara la Afrika.
“Ni jambo la kufurahisha na
kujivunia sana kwamba, kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Utamaduni, Sanaa
na Michezo ya Tanzania na Ubalozi wa
Italia uliopo jijini Dar es Salaam, tumefanikiwa kuwatambulisha wasanii wa
Tanzania kwenye Kamati ya Uteuzi ya Venice Biennale, ambayo ilielewa kiini cha
utamaduni wetu na kukubali maombi yetu, alieleza Mheshimiwa
Mahmoud Thabit Kombo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Italia. Kwa kupata nafasi ya banda kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Venice mwaka
2024, tayari ni ushindi kwa sanaa ya taifa letu ikizingatiwa kuwa ni Maonesho
maarufu duniani ambayo yataleta heshima kubwa na mwonekano wa kimataifa kwa
nchi yetu."
Maonesho ya 60 ya Kimataifa ya Sanaa
ya Venice mwaka 2024 yana kauli mbiu isemayo "Wageni kila Mahali".
Kwa muktadha ambao kazi zitawekwa katika ulimwengu uliojaa migogoro mingi,
inayoakisiwa katika sanaa ya kisasa ya Tanzania kupitia nyenzo kama vile rangi,
hatua madhubuti katika matumizi yake, taswira, na nafsi. Vipengele hivi
havitengani na historia au uzoefu lakini vinapata nguvu ya kujiepusha na
maelezo na maumbo safi.
"Ushiriki wetu kama nchi
katika Maonesho ya 60 ya Kimataifa ya Sanaa ya
Venice mwaka 2024, Dkt. Damas
Daniel Ndumbaro (Mbunge), Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa
Tanzania, alieleza kuwa ni ishara kwamba sanaa ya Tanzania inastahili heshima
ya kimataifa na tuko hapa kuonesha hivyo. Natoa wito kwa wasanii wetu
kuhakikisha wanatumia kikamilifu vipaji vyao kwani hii ni fursa kwao
kujitangaza na kutafuta masoko ya kimataifa.
Serikali ya Tanzania chini ya
uongozi wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuunga mkono ushiriki wa
wasanii wetu katika jukwaa hili muhimu sana ikiwa ni sehemu ya maendeleo na
ukuaji wao ambao hatimaye utawasaidia kupenya katika soko la kimataifa".
Ushiriki wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa ya Venice mwaka 2024, ni
hatua muhimu kwa tasnia ya sanaa ya bara hili na kutoa fursa ya kushiriki
utamaduni na ubunifu wake na hadhira ya kimataifa.
Kwenye Maonesho ya 60 ya
Kimataifa ya Sanaa ya Venice mwaka 2024,
wasanii watakaoiwakilisha Tanzania ni
wanne (4):
- Lutengano Mwakisopile (Lute):
Alizaliwa tarehe 26 Julai, 1976, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ofisi yake ipo
mtaa wa Morogoro Store Oysterbay, jijini
Dar es Salaam. Anaeleza mawazo yake kupitia vifaa mbalimbali kama vile penseli,
makaa, rangi na brashi, turubai, karatasi, au michoro kwenye mbao. Ubunifu wake
usio na mipaka unatokana na mawazo, kumbukumbu, uzoefu, matumaini, na
matarajio.
- Happy Robert: Msanii wa picha aliyezaliwa tarehe 30 Aprili,
1989, huko Songea, mkoani Ruvuma. Kwa sasa anaishi na kufanya kazi jijini Dar
es Salaam. Happy alifanya kazi kama Afisa Utawala katika taasisi mbili tofauti
za binafsi kabla ya kuamua kufuata mapenzi yake ya sanaa na kuwa msanii huru
kuanzia mwaka 2014.
- Naby: Mtaliano, mzaliwa wa Bologna, na ambaye, pamoja na
wenzake wa Kitanzania, wanawakilisha vyema tasnia hii kupitia kazi yao ya
kisanii iitwayo "Vioo Vilivyogeuzwa". Anatumia vyombo vya habari na vifaa
mbalimbali kama vile karatasi na michoro kuanzia usakinishaji mkubwa hadi kazi
za ndani zaidi zinazochochewa na kuficha.
- Haji Chilonga: Alizaliwa mwaka 1969 huko wilayani Masasi, mkoani Mtwara uliopo kusini mashariki mwa Tanzania. Anatoka katika familia ya wahunzi upande wa baba yake na wafinyanzi upande wa mama yake. Kipaji cha Chilonga kiligunduliwa mapema, alipoingia shule ya msingi.
"Vioo Vilivyogeuzwa,",
jina la kazi ya kisanii kwenye banda la Tanzania, hufanya kazi mbili: jozi
mbili za kwanza za vioo zinaoneshana hadithi nne za vipindi vinne tofauti vya
kihistoria, vilivyowasilishwa na wasanii wanne waliochaguliwa.
Msanii wa Zanzibar, Yahya Mzee Mwinyikombo, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wafanyakazi za Mikono
Zanzibar pia atakuwepo na kushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa ya
Venice mwaka 2024.
0 Comments