Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 9 Mei, 2024 wakati akifungua warsha ya Wakuu
wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mikoa
tisa ya Tanzania Bara kuhusu Usimamizi na Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya
Haki Jinai iliyofanyika Jijini Dodoma.
“Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi dumisheni amani na
mshikamano katika maeneo yenu ya kazi na kati yenu na wananchi ili kujenga
taswira nzuri”amesema na kuongeza kuwa inasikitisha kuona viongozi
wanaofanya kazi pamoja hawaelewani na hivyo kusabisha migogoro mahali pa kazi
na pengine kusababisha hasara kwa Serikali.
Amesisitiza umuhimu wa viongozi kutekeleza majukumu yao na kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa, kushirikiana na Taaisi za Haki Jinai na kujipanga kutekeleza Mkakati wa Kubaini Uhalifu kabla hajatendeka badala ya kusubiri kukabiliana nao.
“Wekeni mkakati thabiti wa kuzuia migogoro ya ardhi na endeleeni kuweka
utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyiakazi kwa kuzingatia
sheria, Tatueni kero za wananchi kwa haki bila kumuonea mtu.” Amesisitiza Dkt.
Biteko
Ameongeza kuwa mada mbalimbali zitawasilishwa na wabobezi kutoka sekta
tofauti, hivyo walengwa wajipange kupata maarifa na kuzingatia yote
watakayoelekezwa katika warsha hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa
kazi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, Mhe. Zainab Katimba amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kuunda Tume ya Haki Jinai na kuwa Ofisi yake ipo tayari kuhakikisha azma ya
Rais Samia inafanikiwa.
Awali akitoa maelezo kuhusu matokeo ya Tume ya Haki Jinai, Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya Haki Jinai, Inspekta Jenerali wa Polisi
Mstaafu, Said Mwema amesema kuwa ripoti hiyo inaonesha kuwa wananchi wamekuwa
na maoni mbalimbali ikiwemo malalamiko yanayohusu Serikali za Mitaa ambayo ni
urasimu, huduma duni, ukosefu wa maadili, vitendo vya rushwa na migogoro ya
ardhi baina ya wakulima na wafugaji na wananchi na taasisi za Serikali pamoja
na ukamataji wa watuhumiwa bila kuzingatia utaratibu wa haki zao na misingi
katika kukamatwa kwao.
Warsha hiyo kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa
Halmashauri kutoka Tanzania Bara imehudhuriwa na washiriki kutoka mikoa tisa ya
Arusha, Geita, Kilimanjaro, Mara, Simiyu, Shinyanga.
0 Comments