Madaktari bingwa 60 watua Kigoma


Madaktari bingwa 60 kutoka hospitali za kanda ya magharibi wanatarajia kuweka kambi ya kibingwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Maweni wakishirikiana na madaktari bingwa wa Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Leo tarehe 3 Mei 2024, na mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye imesema huduma hizo zitatolewa kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 6 hadi 10 Mei 2024

Taarifa hiyo imeeleza kuwa madaktari bingwa kutoka hospitali za kanda za Kitete, Katavi, na Sumbawanga watajumuika na madaktari bingwa wengine kwaajili ya kutekeleza huduma hizo.


Akitoa taarifa hiyo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wananchi wa mikoa yote kufika katika hospitali ya Maweni nadnibya muda uliopangiliwa kwani wapo ambao huwa wanafika kupata huduma baada ya mabingwa kuondoka.


Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Maweni akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi mdogo wa ofisi ya mkuu wa mkoa mara baada ya taarifa kwa umma.

Akizungumza baada ya taarifa hiyo Stanley Binagi mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Maweni amesema huduma za kibingwa zinazotolewa hospitalini hapo zinasaidia kuboresha huduma za afya zinazojumuisha vifaa tiba pamoja na na


“Makambi ya kibingwa yamekuwa kichocheo kikubwa cha kuboresha huduma za afya, tumekuwa tukibaini mapungufu yaliyojitokeza kutoka kambi moja hadi nyingine na kuyafanyia kazi, hii imetusaidia sana maana mpaka sasa tumekuwa na vifaa tiba vingi na vya kisasa pamoja na dawa kwaajili ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali, kwa mfano tumefanikiwa kununua mashine mpya ya kisasa ya kufanya upasuaji wa macho” amesema Binagi


Amesema uwepo wa huduma za kibingwa husaidia madaktari wa hospitali hiyo kuongeza ujuzi  na taaluma katika magonjwa mbalimbali na hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.


Mganga mfawidhi Binagi amesema katika kambi hiyo wanatarajia kuwafikia wananchi kati ya 2000 na 3000 watakaohudumiwa na kwamba hata watu wenye uwezo mdogo walioshindwa kufika katika hospitali kubwa za Bugando na Muhimbili watahudumiwa mkoani humo na kuwataka wananchi kuchukua namba mapema kwaajili ya kupata huduma kwa wakati.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo huduma za kibingwa zitakazotolewa na madaktari hao ni pamoja na ubingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi, watoto, upasuaji, magonjwa ya ndani, upasuaji mifupa, dharura na ajali, radiolojia, huduma za afya ya akili  huduma za utengemao, huduma za macho na huduma za kinywa na meno.


Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize.


Post a Comment

0 Comments