Mh. Songe ataka wizara ya uchukuzi kuipa fedha za kutosha TPA

 

Sehemu ya bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika

Mbunge wa Busega Mh. Simon Songe ametoa rai kwa wizara yan uchukuzi pamoja na wizara ya fedha kurudisha mapato ya bandari kwa TPA ili kuboresha na kuimalisha ubora wa Bandari nchini Tanzania.

Rai hiyo ameitoa leo wakati akichangia hoja ya bajeti ya wizara ya uchukuzi katika Bunge la 12 linaloendelea jijini Dodoma

Amesema kumekuwa na changamoto nyingi zinazo jitokekeza katika bandari baada ya mapato yanayo patikana kupitia TRA kutumika katika sekta nyinginezo na kisha zinazo bakia kuwekwa katika mfuko.

Amebainisha baadhi ya changamoto wanazo kumbana nazo ni kuchelewesha kulipa wakandarasi pamoja na kushindwa kukarabati miundo mbinu  kwa wakati

“TPA wanapata fedha kidogo na hazitoshi.” Amesisitiza Simoni

Mh. Songe amehitimisha mchango wake kwenye bajeti ya uchukuzi kwa kuiomba serikali kulipa fidia kwa wananchi wa   Bariadi Simiyu waliyo pisha ujenzi wa uwanja wa ndege

Amesema baadhi ya wananchi wanaishi maisha magumu na wengine kuishi kama wakimbizi kwa kukosa maeneo maalumu ya kuishi kwa sababu ya kucheleweshewa fidia zao.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mh. Ester Matiko ameiomba serikali kujenga uwanja wa ndege katika hifadhi ya Serengeti ili kuondoa adha ya changamoto ya usafiri kutoka hifadhi moja hadi nyingine.

Amesema kumekuwa na changamoto kubwa wanayo kumbana nayo watalii na wananchi wanapo toka mkoa mmoja kwenda mkoa wa Mara kulazimika kutumia usafiri wa magari ambayo pia miundo mbinu yake sio rafiki.

Ameleza kuwa kumekuwa na miundo mbinu mibovu ya bara bara inayo pelekea watalii wengi kutumia mda mrefu kwenda katika hifadhi ya Serengeti pamoja na kutembelea katika kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Jullius Nyerere.

Mwandishi: Sara Mataro

Mhariri: Prosper Kwigize

 

Post a Comment

0 Comments