Mradi wa Binti na Hedhi salama wazinduliwa Kigoma

Shirika la Africraft linalotoa huduma za afya na mazingira limeungana na wadau wengine pamoja na serikali kutatua changamoto zinazowakabiri watoto wa kike kiafya na kimazingira ikiwemo kukabiliana na ukosefu wa taulo za kike kwa wanafunzi nchini Tanzania.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi wa Binti pamoja na madhimisho ya siku ya Hedhi salama duniani ambayo huadhimishwa kila may 28  Mkurugenzi wa AfriCraft amesema vyuo vya ufundi vimekuwa vikisahaulika kupewa elimu ya upatikanaji Hedhi salama jambo ambalo limewasukuma  kutoa elimu ya uboreshaji wa taulo za kike 

Aidha Meneja mradi kutoka AfriCarft Aneth Kiyao amesema Mradi huo unatarajia kuwafikia zaidi ya wanafunzi wa kike elfu 12 pamoja na Vyuo 15 katika mikoa 7 ya Tanga,K igoma, Dar es salaam, Morogoro, Rukwa, Lindi na Zanzibar huku kwa mkoa wa Kigoma ukitarajia kuanza kufanyika katika Manispaa ya Kigoma Ujiji

Changamoto ya hedhi salama kwa watoto wa Kike katika shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo vya ufundi katika maeneo mbalimbali nchini imekuwa kikwazo katika maendeleo ya msichana kiafya  na ustawi katika maendeleo ya Jamii 


Kwa upande wa wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali wamezitaja changamoto za usalama wa Taulo za kike zenye kuwafanya kuwa huru katika shuguli mbalimbali zikiwemo za michezo ,Kukosekana na vyumba maalum vyuoni pamoja na Gharama katika kununua Taulo za Kike 

Akimuwakilisha Afisa Elimu secondari, Afisa Elimu Maalum Manispaa ya Kigoma Ujiji Shingwa Hamis amesema mahitaji ya taulo za kike katika shule za Manispaa hiyo ni makubwa yakiendana na changamoto ya ukosefu wa Vyumba vya kubadilishia Taulo katika shule hizo

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ambaye alimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Kigoma DR. Albert Mwesiga amesema licha ya kuwa ni suala la kibaolojia lakini wamelenga katika kumuinua na kumuwezesha Mtoto wa Kike kupitia Hedhi salama 

Maadhimisho hayo yameambatana na Kauli mbiu isemayo “Pamoja kwa Hedhi Rafiki Ulimwenguni “huku kauli mbiu ya Mradi ikiwa ni Uwezeshwaji wa msichana kupitia Hedhi salama”.

Post a Comment

0 Comments