Rais Samia ampongeza msanii Harmonize


AMPA SHUMBE HARMONIZE0, KUFUNGUA FURSA ZAO LUFUFU NJE YA NCHI*


Anaaandika Mshititi Dkt.Ahmad Sovu  


Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewanasihi na kuwataka wasanii wote kua kitu kimoja na kuacha kuzodoana.


Nasaha hizo amezitoa katika  usiku wa Mei 25, 2024 kulikofanyika uzinduzi wa album mpya ya msanii HARMONIZE kunako ukumbi wa Mlimani City huko Jijini Dar es Salaam.


Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema atahakikisha anawapatia fursa zaidi za mafunzo nje ya nchi wasanii wote.


Mbali ya fursa ya mafunzo, amesema atakuwa akienda nao katika safari mbalimbali zitakazokuwa na shughuli mahususi ziwahusuzo.


Aidha, amewasisitiza wasanii kutokukata tamaa na kuwa focus katika malengo yao.


Heko kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki katika matukio haya na kuwaunga mkono vijana.


sovu82@gmail.com

Post a Comment

0 Comments