Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kujenga
uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani katika msingi wa viwanda,
huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.
Aidha, Rais Samia amesema sekta
ya viwanda inaongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa wananchi, jambo ambalo ni
muhimu katika kukuza uchumi jumuishi na kusaidia katika mapambano ya kuondoa
umasikini.
Rais Samia amesema hayo leo
wakati akizindua kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Saturn
Corporation Limited kilichopo wilaya ya Kigamboni.
Vile vile, Rais Samia amesema
kiwanda hiki ni chachu ya ukuaji wa viwanda
na sekta nyingine kwa kuwa kinatumia
vioo vinavyozalishwa na kiwanda kingine, ambacho zaidi ya 80% ya malighafi zake pia zinapatikana hapa nchini.
Hivyo, matumizi ya bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini yanapunguza gharama kwa kampuni yenyewe inayotengeneza magari na
pia inaongeza manufaa ya uwepo wa kampuni hiyo kwa uchumi wa nchi.
Kiwanda hiki kitatoa ajira za
moja kwa moja takribani 250 na zisizo za moja kwa moja 1,800,
kuongeza mzunguko wa fedha, mapato ya serikali
na kuhaulisha teknolojia.
0 Comments