Mkuu wa mkoa Kigoma Mh Thobias Andengenye ameelekeza
chama cha wafanyakazi mkoa TUCTA kuwachukulia hatua kali za kisheria waajiri
watakao bainika kunyanyasa na kuwakandamiza watumishi wao.
Agizo hilo amelitowa
katika hotuba yake siku ya maadhimisho mei mos ambayo kimkoa
yamefanyika jana katika uwanja wa umoja
wilayani Kasulu.
Amesema kuwa yapo malalamiko mengi kwa baadhi ya waajiri
kuwakandamiza wafanyakazi wao katika mazingira ya kazi jambo ambalo ni kinyume
cha sheria na pia ni utovu wa nizamu
Ameeleza kuwa ni vyema kwa mtumishi kutoa taarifa kwenye
mamlaka husika kuhusu vitendo hivyo ili wamchukulie hatua za kisheria
atakayebainika kukiuka kanuni za ajira
Sambamba na hilo amekemea vikali uzembe kazini pamoja
wafanyakazi kuto toa ushirikiano mzuri kwa wananchi wanao tegemea huduma bora
kutoka kwao.
Awali akisoma risala ya wafanyakazi katibu wa shirikisho
la vyama vya waanyakazi (TUCTA) mkoa wa Kigoma Bw. Jumanne Magulu amesema kuwa moja
ya changamoto inayo wakabili waajiriwa wengi ni kukandamizwa wakati wa majukumu
yao.
Amesema waajiriwa wengi wamekuwa wakinyanyaswa na kushindwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika kwa kuhofia kusimamishwa au kufukuzwa kazi.
Baadhi ya watumishi walio hudhuria katika maadhimisho
hayo ambao majina yao hawakupenda kutajwa wamekiri kuwepo kwa vitendo vya
ukandamizaji na manyanyaso kutoka kwa waajiri
Wamesema watumishi wa kike ndio wanakabiliwa na
changamoto nyingi hususani unyanyasaji wa kingono.
Bi. Rose Marry Castor ambaye ni mkazi wa Heru juu na mjasiriamali
akizungumza na Buha News amelalamikia kuwepo kwa uzembe miongoni mwa
wafanyakazi wa taasisisi za Umma na ameomba watumishi kutambua majukumu yao
wawapo kazini na kufanya kazi kwa kujali misingi ya taaluma zao.
Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakitanguliza
rushwa kwanza ndipo watoe huduma kwa wakati jambo ambalo kwa wanyonge na wasio
jiweza hushindwa kupata huduma.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani 2024
imekuwa na kauli mbiu isemayo “Nyongeza ya Mashahara ni msingi wa mafao bora nak
inga dhidi ya hali ngumu ya Maisha”
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments