Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa maagizo kwa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuwaruhusu wakulima waliolima katika hifadhi la pori la Kagera Nkana {Makere Kaskazini} wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma Kwenda kuvuna mazao yao kisha kusitisha kulima katika hifadhi.
Agizo hilo
limetolewa Bungeni leo kufatia swali lililo ulizwa na Mbunge wa viti maalum
mkoa wa Kigoma Mh. Josephina Genzabuke akihoji nini tamko la serikali kuhusu
wakulima walio zuiliwa na TFS kuvuna mazao yao katika pori la hifadhi la Kagera Nkanda.
Mh. Genzabuke
amebainisha kuwa wakulima kutoka vijiji kurugongo, kaburanzwiri, Kagerankanda,
Mvinza Nyakitonto, Mgombe, Nyachenda na Kitagata vya wilaya ya Kasulu wamezuiliwa
kuvuna mazao yao hali inayohatarisha ustawi wa jamii hiyo.
Akitoa
azimio la wizara ya Mali asili nan Utalii naibu Waziri wa mali asili na utalii Mh.
Danstan Luka Kitandula ameagiza TFS kuruhusu kwa wakulima waliolima katika hifadhi
za misitu wilayani Kasulu kuvuna na kisha wazuiliwe wasiendelee kulima katika
misitu ya taifa.
“Tulishatoa
maelekezo kwa wakala wa misitu Tanzania TFS kuwaruhusu wakulima hao kuvuna
mazao yao na kisha wazuie asiwepo mkulima atakayeingia hifadhini kufanya
shughuli hizo tena, sasa nitumie Bunge hili tukufu kuwaagiza TFS watoe kibali
kwa wakulima wakavune nah atua zichukuliwe wasilime tena” amesisitiza Kitandula
akizibu swali la nyongeza la mh. Genzabuke.
Hivi
Karibuni diwani wa Kata ya Kurugongo Edson Hanyuma aliongoza wakulima zaidi ya
30 kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kasulu kuomba waruhusiwe kuondoa mazao yao
katika mashamba waliyolima ndani ya misiti kufuatia TFS kupiga marufuku
shughuli za uvunaji
Akiongea na
buha News Mh. Hanyuma baada ya Bunge kuagiza wakulima kuruhusiwa ameipongeza
serikali kwa kauli hiyo akitaja kuwa agizo limetoa faraja
kwa wakulima wengi wilayani Kasulu.
Ameeleza
kuwa tabia ya wakulima kuendelea kulima katika hifadhi hiyo kunatokana na
kukosa maeneo maalumu ya kilimo na hivyo kujikuta katika mgogoro na TFS.
Amefafanua
kuwa endapo serikali itatenga eneo maalum kwa ajili ya wakulima hao itasaidia
kuondoa changamoto ya wakulima kuingia katika hifadhi.
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments