Serikali ya
Tanzania imetangaza kukamilika kwa taratibu za uandaaji wa mswaada wa marekebisho
ya sheria ya ndoa yam waka 1971 itakayozuia msichana kutoolewa kabla ya umri wa
miaka 18 baada ya kukusanya ukusanyaji wa maoni na mapendekezo ya wananchi.
Hayo
yemebainishwa leo na Naibu Waziri wa katiba na sheria Mh. Jumanne Sagini wakati
akijibu swali lililo ulizwa na Mbunge wa viti maalumu Mh. Dr. Thea Medad Ntala akihoji
lini serikali italeta mswada wa sheria ya ndoa ili kukabiliana ya ndoa za
utotoni.
Mh. Jumanne
Sagini amesema baada ya baada ya maamuzi ya Mahakama ya Tanzania, serikali
iliwasilisha mswada wa marekebisho ya sheria ndogo kupitia tangazo namba moja la
mwaka 2021 ilipendekeza umri wa ndoa kuwa miaka 18.
Amesisitiza
kuwa Bunge kupitia kamati ya uongozi ilielekeza serikali kukusanya maoni ya
wananchi kuhusu sheria hiyo na tayari hatua mbalimbali za ukusanyaji wa maoni
zimetekeleza ikiwemo kufanyika kwa kongamano la sheria ya ndoa lililofanyika
April 26 mjini Dodoma.
Kwa upande
wake Mhe. Ester Maleko Mbunge wa viti maalumu akiuliza swali la nyongeza
amehoji kuhusu lini serikali itafanya marekebiso ya sheria ya ndoa kipengeze
cha utatuzi wa migogoro ya ndoa na matunzo kwa Watoto
Serikali
kwa upande wake imebainisha kuwa yameshaundwa mabaraza ya usuluhishi ambapo
moja ya kazi zake ni kutatuza migogoro ikiwemo matunzo ya watoto.
Naibu
Waziri wa katiba na sheria Mh. Jumanne Sagini amekiri kuwa sheria ya ndoa ya
mwaka 1971 kuhusu migogoro na fidia za matunzo ya watoto ina mapungufu kadhaa
hasa kwenye viwango na anatoa maagizo kwa tume ya kurekebisha sheria katika
maboresho yanayoendelea wazingatie pia suala la viwango vya fidia hizo
Aidha
ametoa wito kwa wananchi ambao wataona au kukabiliwa na changamoto katika
utekelezaji wa sheria hiyo wende mahakamani kudai haki zaidi.
Mwandishi:
Sara Mataro
Mhariri:
Prosper Kwigize
0 Comments