Wafungwa wafikiwa na maboresho ya Daftari la Kudumu la wapiga Kura

Wakati wa Uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la kupiga kura ukitarajiwa kufanyika Julai Mosi, 2024, wafungwa waliohukumiwa chini ya miezi sita watashiriki katika mchakato wa uboeshaji wa taarifa zao.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Mei 29, 2024, manispaa ya Kigoma Ujiji mkurugenzi wa uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhan Kailima, amesema wafungwa hao na wanafunzi wa vyuo vikuu watafikiwa kwa mujibu mujibu wa kanuni ya 15(2)(c) cha kanuni ya uboreshaji wa daftari la kupiga kura kwa mwaka 2024.

Amesema kutakuwa na jumla ya vituo 130 vitakavyokuwa magerezani kwaajili ya kuhakiki taarifa za wafungwa hao.

Katika uboreshaji wa taarifa hizo unatarajiwa kukamilika Machi 2024 na kwa kuzingatia matokea ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kutakuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 18 la wapiga kura kutoka wapiga kura milioni 29,754,699 wa mwaka 2020 hadi kufikia wapiga kura 34,746,638 kwa mwaka 2024.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma katika ukumbi wa mkuu wa mkoa

Amesema kati ya hao, wapiga kura milioni 4,369,531 wanatarajia kuboresha tarifa zao na 594,494 wataondolewa katika Daftari kwa kupoteza sifa za kuwa wapia kura.

Kwa upande wa mkoa wa Kigoma mkurugenzi wa uchaguzi amesema kutakuwa na ongezeko la wapiga kura wapya 224,355 kutoka wapiga kura 1,043,281 kwa mwaka 2020 hadi kufikia wapiga kura 1,267,636 kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 21.5 ya wapiga kura waliopo kwenye daftari.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema kwa mkoa huo vituo 1,162 vitatumika kwenye uboreshaji wa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 69 katika vituo 1,093 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kailima tume tayari imekamilisha maandalizi kwaajili shughuli hiyo ikiwa ni pamoja na uhakiki wa wa vituo vya kuandikisha wapiga kura ambapo vituo 40,126 vitatumika katika uboeshaji huo, huku 39,709 vikiwa Bara na 417 vikiwa Zanzibar.

Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize 

Post a Comment

0 Comments