Wahitimu wa JKT wapewa tahadhari ya matumizi ya simu janja


Mkuu wilaya ya Kigoma, Salum Kalli, amewataka wahitimu wa  kujenga taifa kutoka 821KJ Bulombora iliyopo halmashauri ya wilaya ya Kigoma kuwa makini na matumizi ya simu ganja katika mitandao ya kijamii.


Amesema amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya operation” ya kujitolea ya miaka 60 ya JKT katika kambi ya Bulombora mkoani Kigoma ambapo amesisitiza kuwa vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kiteknolojia


Bw. Kalli amehimiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia simu janja zimekuwa chanzo cha kujifunza na kufahamu mambo mbalimbali yanayoendelea katika dunia na kuwataka wahitimu hao wasikubali kuvurugwa nazo bali wazitumie katika kujifunza vitu vya msingi kwa ajili ya ulinzi wa taifa.


“Vijana wengi hawana elimu ya matumizi sahihi ya simu ganja na mitandao ya kijamii ,wanatumia simu kutazama vitu visivyofaa na kurusha maudhui yanye madhara katika mitandao, nawaasa msimtumie vibaya, yeyote atakayebainika atachukulia hatua mara moja” Amesema DC Kalli


Mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli akihutubia wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Tiafa katika kambi ya Bulombora mkoani Kigoma. Picha na. Adela Madyane

Amesema“elimu na mafunzo mliyopata myatumie kulinda mipaka ya nchi, msikubali nchi yenu ilindwe na mtu mwingine, msimamie kiapo, nidhamu iwe kitu pekee katika kila kitu mnachokifanya, msimamie miongozo ya nchi ili kutimiza lengo la taifa la kuwafanya kuwa jeshi la akiba”.


Akiongea mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Hassan Mabena ambaye pia ni mkuu a tawi la Utawala wa jeshi hilo amesema vijana waliohihitimu mafunzo ya awali wanapaswa kujikita katika misingi ya  “operation” ya kujitolea ya miaka 60 ya kujenga taifa ili kutekeleza malengo ya mwasisi wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Brigedia Hassan Mabena mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) akitoa ujumbe wa mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele wa kuwataka wasijiingingize katika makundi ya vijana wavuta bangi na wanaotumia madawa ya kulevya 

Mabena amewataka vijana hao kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu wa kujiunga na JKT kutokana na mafunzo ya uzalendo na stadi mbalimbali za maisha wanazozipata zinazowaepusha vijana wengi kuingia katika makundi yanayoharibu mustakabali wa maisha yao.


Mafunzo hayo ya awali yamedumu kwa miezi minne toka mwezi Disemba 2023 hadi Aprili 2024 ambapo hatua inayofuata ni mafunzo ya miezi 20  ya stadi za kazi na stadi za maisha  katika makambi tofauti kote nchini.


Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize





 

Post a Comment

0 Comments