Breaking New: Uteuzi na Utenguzi wa viongozi wa serikali

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

 

   i.          Amemteua Dkt. Ashura Abdul Katunzi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi, Dkt. Katunzi alikuwa Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Dkt. Katunzi anachukua nafasi ya Dkt. Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

 

 ii.          Amemteua Bw. Hassan Juma Mnyika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Kabla ya uteuzi, Bw. Mnyika alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu. Bw. Mnyika anachukua nafasi ya Bw. Lain Ephraim Kamendu ambaye amestaafu.

 

iii.          Amemteua Bw. Addo Missama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi. Kabla ya uteuzi, Bw. Missama alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu. Bw. Missama anachukua nafasi ya Bw. Joseph Constantine Mafuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

 

 

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments