CHADEMA wapata Pigo, Mchungaji Msigwa atimkia CCM

 


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ajiunga Rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM) Jijini Dar es Salaam 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan amempokea msigwa leo mbele ya ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ikulu jijini Dar es Salaam

Msigwa ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ameonekana shujaa katika anga la siasa za Tanzania mara baada ya kutangaza rasmi kujiunga na CCM wakati wa Kikao cha NEC Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2024. 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akitabasamu wakati katibu mkuu wa CCM Dr. Emanuel Nchimbi akimuingiza ukumbini mchungaji Msigwa.

Mchungaji Peter Msigwa (mwenye nguo nyeusi) akisalimia wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM akiongozwa na Katibu mkuu Dr. Emanuel Nchimbi

Mchungaji Msigwa aliwahi pia kuwa Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema pamoja na kushuka Nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama hicho. 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa na Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema Mchungaji Peter Msigwa akizungumza mara baada ya kutangaza rasmi kujiunga na CCM wakati wa Kikao cha NEC Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2024.

Mchungaji Msigwa ni mmoja wa viongozi wa kisiasa waliokuwa wakiaminiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye hivi karibuni aliandikwa na vyombo vya habari akihusishwa na mgogoro wa kupinga matokeo ya michakato ya uchaguzi ndani ya chama chake cha zamani.

Ndani ya CHADEMA kunatajwa kuwepo na fukuto la kutoaminiana miongoni mwa viongozi wakuu wa chama dhidi ya waliokuwa wanaharakati na wabunge wa zamani wa chama hicho, huku sakata la wabunge 19 wa viti maalumu ambaoo walifukuzwa na chama hicho wakiendelea na vikaoo vya bunge kama kawaida.

Imeandikwa na. Mwandishi wetu - CCM

Post a Comment

0 Comments