Wananchi wa wilaya ya
Kasulu mkoa wa Kigoma wametakiwa kulinda na kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda
miti lafiki ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi.
Agizo hilo limetolewa
leo katika kata ya kumunyika na mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Issack Antony
Mwakisu wakati akizindua mradi wa maji uliowezeshwa na shilika la Hope Foundation
katika mtaa wa Sunzu na Nyerere
Kanali Mwakisu amesema kila mwananchi anao wajibu wa kulinda na kutunza chanzo cha maji sambamba na kuacha kufanya shughuli za kijamii karibu na vyanzo hivyo.
Amesisitiza kuwa
maeneo yote yenye vyanzo vya maji yanapaswa kuachwa kwanumbali wa mita 60 na sheria kali
itachukuliwa dhidi ya wananchi watakao kutwa wanafanya shughuli za ndani ya mita 60.
” Maji ni uhai tuyatunze yatutunze kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa hiki ni kipindi cha kiangazi tunapashwa kulinda vyanzo” amesema Mwakisu
Kwa upande wake
mkurugenzi wa shirika la Hope Foundation Bi. Evelin Amos amesema taasisi yake imejikita katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na
salama.
Amesema mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi million 4 ambazo zimepunguza kero ya maji kwa jamii mjini katika kata ya Kumnyika
Awali, mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya mji wa Kasulu amewataka wananchi kutunza mji wa kasulu kwa
kufanya usafi katika mazingira ya nyumbani kwenye vyanzo vya maji na maeneo ya
biashara ili kuweka mji wa kasulu katika hali ya usafi.
Amesema kuwa ili mji
wa kasulu upendeze umapaswa kuwa safi mda wote hivyo kila mwananchi anawajibu
wa kutunza mazingira
Uzinduzi wa mradi maji katika kata ya Kumnyika limeambatana na zoezi la usafi ambalo limeongozwa na mkuu wa wilaya Mh. Issack Mwakisu wakianzia mtaa wa highway hadi ofisi ya mamlaka ya mapato TRA wilayani Kasulu.
Mwandishi. Sara Mataro
Mhariri. Prosper Kwigize
0 Comments