DC Kasulu akerwa na ongezeko la vitendo vya ukatili

Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa vyombo vya dola katika kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vile ulawiti na ndoa za utotoni vinavyozidi kuongezeka wilayni Kasulu mkoani Kigoma.

Agizo Hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Issack Mwakisu wakati akihutubia baraza la madiwani  katika ukumbi wa halmashauli ya mji kasulu.

Kanali Mwakisu amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya ulawiti, ubakaji, na uporaji wilayani humo.

" Juzi nilikuwa Mwilamvya Kuna kaka amelawitiwa jambo hilo linaninyima usingizi naomba madiwani Kwa pamoja tuwe mstari wa mbele kupambana na uovu huu" amesema Kanali Mwakisu.

Pia amekemea vikari suala la kuwaajiri watoto wenye umri mdogo ambao wanatakiwa kupewa haki Yao ya kupata elimu.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Murusi Mh. Fanuel Kisabho amekili kuongezeka Kwa matukio hayo hasa katika kata yake yenye soko maarufu la "Kwa Shayo" hali inayo pelekea hofu zaidi kwa wananchi.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria na adhabu kali kwa wahusika wa vitendo hivyo kumekuwa na desturi ya wananchi kuwaficha watuhumiwa Kwa lengo la kuyamaliza wao wenyewe bila ya kufuata sheria

Aidha Diwani wa viti maalum tarafa ya Heru Chini Mh. Nell Nashon Kibamba ameshauri kuwa ili kupambana na vitendo vya ukatili serikali inapaswa kuongeza vituo vya polisi na ustawi wa jamii karibu na jamii na elimu itolewe kwa wananchi kupitia vituo vya redio semina, makanisani na misikitini.

Mwandishi: Sara Mataro

Post a Comment

0 Comments