Joto la CAG linafukuta Kasulu, RC Kigoma atoa maagizo mazito

Watumishi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kufikia June 30 wawe wamekamilisha utekelezaji wa hoja zilizo tolewa na na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali  CAG.

Agizo hilo limetolewa jumatano wiki hii na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye katika Baraza la Madiwani lililofanyikia katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu 

Mh. Andengenye amesema hata vumilia uzembe unaojitokeza kwa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakae bainika kutotekeleza.

Amesema kufikia june30 hoja zote ziwe zimefungwa na zimefanyika Kwa utalatibu husika ili isitoke hati chafu Kwa kua mkoa umekuwa ukipata hati safi mara tatu mfululizo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akisoma makarasha wakati wa kikao mahususi cha kujadili taarifa ya CAG wilayani Kasulu

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kasulu Kanal Issack Mwakisu amesema watumishi na wakuu wa idara wanapaswa kushirikiana pamoja na mkaguzi wa hesabu za selikali ili kuboresha uwajibikaji na huduma bora kwa jamii

Awali akisoma taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw. Semistatus mashimba amebainisha kuwa halmashauri hiyo ilipata hati yenye mashaka katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2023/2024

Pamoja na maagizo ya mkuu wa mkoa  wa Kigoma, Mwenyekiti wa halmashauri ya wiaya ya Kasulu Bw. Eliya Kagoma amemtaka mkurugenzi kuwasimamia watumishi ipasavya na kukakikisha maelekezo ya CAG yanafanyiwa kazi haraka na kwa weledi

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Mbelwa Abdallah anewataka watumishi wa serikali za mitaa kutambua kuwa CAG sio adui wa halmashauri na wanapaswa kumpa ushirikianao.

"Wakaguzi sio adui wa halmashauri tunapawa kumpa ushilikianao kuhakikiaha mwaka uu hatipati hati chafu" amesema Mbelwa

Mwandishi: Sara Mataro

Post a Comment

0 Comments