MISA yaomba kupunguzwa ada lesseni vyombo vya habari vya kijamii

Taasisi ya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania(MISA-TAN), imeiomba serikali kupunguza viwango vya ada ya maombi ya leseni na tozo za kuendesha mitandao ya kijamii(Blogs, Online Tv na Rafio ili kuvutia vijana wengi kumiliki wenye taaluma ĺ kisheria.

MISA pia imeomba serikali kuharakisha kuunda baraza huru la habari na mfuko wa kusaidia wanahabari nchini kujiendeleza kielimu.

Mjumbe wa bodi ya MISA-Tan,Mussa Juma ametoa wito huo leo June 26, wakati akifunga Warsha ya waandishi wa habari na wadau wa habari kujadili kanuni za maudhui ya mtandaoni za mwaka 1998 na maboresho yake katika hotel ya Silver sand kunduchi jijini Dar es salaam.

Mussa Juma mjumbe wa bodi ya MISA Tanzania akitoa mada kuhusu changamoto ya gharama za kuendesha vyombo vya habari nchini Tanzania


Juma alisema, gharama.ya sh 500,000 ya lesseni ua kumiliki blogs na millioni mona kumiliki luninga za mtandaoni ni kubwa kwa vijana na watu wenye ulemavu.

"Kama ada ya lesseni ikiwa ndogo vijana wengi wenye taaluma ya habari na TEHAMA watamiliki mitandao ya kijamii kisheria na kutoa habari"amesema

Amesema kwa sasa kutokana gharama kubwa za leseni karibu robo tatu ya mitandao inaendeshwa  bila lesseni .

Alisema muhimu serikali kupitia TCRA kugawa mitandao ya jamii ambayo inamilikiwa kibiashara na ambayo inafanya kazi ya kutoa elimu na kupashana.habari pekee.

Changamoto nyingine inayotajwa kuwa tatizo kwa tasnia ya habari na umiliki wa vyombo vya habari ikiwemo Radio za Kijamii ni pamoja na serikali kutoza pesa nyingi kwenye maombi ya uanzishaji wa vituo ambapo mhusika hutakiwa kulipa dola 1000 kwa ajili ya maombi na dola 2000 kupata kibali cha Ujenzi na masafa kabla ya malipo ya leseni, jambo linalokwamisha vijana wenye taaluma na wazalendo kuanzisha radio na badala yake wanasiasa na matajiri kuchukua fursa hizo.

Juma  ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari(JOWUTA) na mkurugenzi wa taasisi ya wanahabari ya MAIPAC, pia aliomba serikali kuharakisha kuudwa baraza huru la habari,bodi ya ithibati na mfuko wa kusaidia wanahabari.

Akizungumza kwa niaba ya Msemaji mkuu wa serikali,Mkurugenzi msaidizi wa Maelezo,Patrick Kipangula alisema serikali kupitia TCRA bado inaendelea na utafiti juu ya masuala ya lesseni na ada mbalimbali.

Patrick Kipangula kaimu msemaji mkuu wa serikali nchini Tanzania na afisa wa idara ya habari Maelezo Dar es Salaam


Kipangula hata hivyo aliwataka wanahabari ma wadau wa habari kuheshimu sheria na kanuni za masuala ya habari .

Awali wakitoa mada katika warsha ,Mawakili Gedion Mandes , Afisa programu wa LHRC Raymond Kanegene na Deus  Kibamba walitaka wanahabari na kusoma kanuni za maudhui ya mitandaoni ili kutovunja sheria

Wakili Mandes pia licha ya kushauri kupunguzwa ada za leseni alitaka elimu zaidi kutolewa juu ya kanuni hizo na kuzingatia haki za makundi ya walemavu.

Wakili Kanegene akichambua kanuni hizo alisema zinamapungufu lakini lazima zifuatwe.

Alibainisha mapungufu ikiwepo kukataza kuandika habari za kuchochea biashara ya kamari mitandaoni wakati serikali ikipokea kodi.

Kwa upande wake Kibamba alisema.lengo la kanuni za maudhui mtandaoni ni kudhibiti usambazaji holela wa habari na taarifa.

Katika kanuni hii kuna mambo mazuri na mabaya hivyo ni muhimu kuzijua kanuni.

Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa MISA TAN Elizabeth Riziki alisema MISA itatumia njia ya majadiliano ma serikali na wadau katika kudai kanuni nzuri za maudhui ya mitandaoni lakini pia sheria bora.

Alisema anaishukuru serikali ya awamu ya sita walau imeboresha baadhi ya sheria na kanuni na imefungua milango ya majadiliano zaidi ili kuboresha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.

Warsha hiyo iliandaliwa na MISA-Tan kwa ushirikiano na Shirika la Protection international Afrika na kudhamiwa na  serikali ya Finland

Zaidi wadau 33 kutoka Tanzania bara na visiwani walishiriki warsha hiyo. 

Imeandikwa na. Mwandishi wetu DSM

Post a Comment

0 Comments