“Uboreshaji wa daftari utazinduliwa hapa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB). Tayari Tume imeamua kwamba uzinduzi huo ufanyike katika uwanja wa Kawawa uliopo hapa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji,” amesema Mhe. Mwambegele.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji.
Wadau wa masuala ya Uchaguzi wakiwa katika mkutano huo Mkoani Kigoma
Viongozi wa Kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi
Watu wenye ulimemavu nao ni wadau muhimu wa masuala ya uchaguzi, hapa mkalimani wa lugha ya alama akimfanyia tafsri mmoja wa washiriki wa mkutano huo. Afisa kutoka Idara ya Daftari akiwasilisha mada
Washiriki wakichangia mjadala uliofanyika baada ya kuwasilisha mada.
.
0 Comments