Wazazi na walezi wa
wanafunzi wa shule za msingi na sekodari wametakiwa kuwapa watoto muda wa
kutosha wa kujisomea badala ya kuwatuma kazi nyingi za nyumbani.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma Mwl Vumilia Julius Simbeye wakati akizungumza na waandishi wa habari
Mkurugenzi huyo
amesema kuwa kila mzazi anao mchango
mkubwa wa kupandisha kiwango cha ufaulu wa mtoto wake kwa kumtengea muda
wakutosha wa kujifunza zaidi katika kipindi cha likizo.
“ Wazazi msitumie muda huu wa likizo ya wanafunzi kuwapa kazi nyingi zitakazo wafanya washindwe kujisomea kwani tutakuwa tunatengeneza kizazi kisicho kuwa na elimu"
Vilevile mwalimu Simbeye ameeleza kuwa kipindi hiki cha likizo mzazi
anapaswa kumlinda mtoto dhidi ya makundi maovu yanayo lenga kudidimiza taaluma ya mtoto
Kwa upande wake mwalim
wa shule ya msingi Nyarumanga iliyo katika kata ya Kigondo wilaya ya kasulu ambae hakutaka jina lake litajwe amekiri kuwepo
kwa ufauru hafifu wa wanafunzi kunakochangiwa na mwamko mdogo wa wazazi katika
masuala ya kitaaluma
“tunapo funga muhula
wa masomo na kuwapa watoto likizo tuna maanisha
kuwa mtoto anapo kuwa nyumbani akajiandae kisaikolojia kwa muhula ujao ili kuongeza kiwango cha
ufaulu kwa kujisomea.” amesisitiza
mwalimu huyo.
Imesisitizwa kuwa ni wajibu wa wazazi kutambua nafasi yao katika taaluma ya mtoto hivyo mtoto apewe nafasi ya kujisomea na kufanya mazoezi ya kitaaluma ikiwa ni pamoja na kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya ya mwili na akili wakati wa likizo
Mwandishi. Sara Mataro
0 Comments