(i)
Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anachukua nafasi ya Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.)
ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(ii) Mhe.
Deogratius John Ndejembi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu);
(iii) Mhe.
Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
(iv) Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Mbunge
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya
uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy, anachukua
nafasi ya Mhe. January Yusuf Makamba (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(v) Mhe. Cosato David Chumi (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe. Chumi anachukua nafasi
ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi;
(vi) Mhe. Deus
Clement Sangu (Mb.) ameteuliwa kuwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
(vii) Mhe. Dennis
Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Mhe. Londo
anachukua nafasi ya Mhe. Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(viii) Bw. Eliakim
Chacha Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kabla
ya uteuzi huu Bw. Maswi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi
wa Umma (PPRA);
(ix) Bi. Mary Gaspar Makondo ameteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Makondo alikuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Katiba na Sheria. Bi. Makondo anachukua nafasi ya Bi. Rehema Sefu
Madenge ambaye amestaafu;
(x)
Bw. Kiseo
Yusuph Nzowa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla
ya uteuzi huu Bw. Nzowa alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu;
(xi) Bw. Musa
Haji Ali ameteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Ali alikuwa Afisa Mwandamizi,
Ofisi ya Rais – Ikulu;
(xii) Bw. Louis Peter Bura ameteuliwa kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Chato. Bw. Bura anachukua nafasi ya Bw. Said Juma Nkumba ambaye amepangiwa majukumu mengine;
(xiii) Bi. Kemirembe Rose Lwota amehamishwa kutoka Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Serengeti;
(xiv) Dkt. Vincent Biyegela Mashinji amehamishwa
kutoka Wilaya ya Serengeti kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya Manyoni;
(xv) Dkt. Maulid Suleiman Madeni ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti;
(xvi) Bw. Afraha Nassoro Hassan amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Serengeti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
Bw. Hassan anachukua nafasi ya Bw. William Anyitike Mwakalambile ambaye uteuzi
wake umetenguliwa; na
(xvii) Bw. Dennis Kwame Simba ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Kabla ya
uteuzi huu Bw. Simba alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania
(TAFICO).
Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
0 Comments