i.
Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb.) ameteuliwa kuwa
Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Jafo alikuwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
ii.
Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa
kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya
uteuzi huu, Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
iii.
Mhandisi Yahya Ismail Samamba ameteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Samamba alikuwa
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Mhandisi Samamba anachukua nafasi ya Bw.
Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.
iv.
Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda
alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Zanzibar (ZRA).
v.
Bw. Alphayo Japan Kidata ameteuliwa kuwa
Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais - Ikulu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kidata alikuwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
MAONI YA WANANCHI
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Buha news kuhusu mabadiliko haya wametaja kuhusishwa na mgomo wa wafanyabiashara katika masoko mbalimbali waliokuwa wakishinikiza serikali kutazama upya mwenendo wa mamlaka ya mapato tanzania unaotajwa kuwakandamiza wafanyabiashara.
Imeelezwa kuwa Uhamisho wa Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji na kamishna wa mamlaka ya Mapato tanzania TRA Bw. Alfayo Kidata ni sehemu ya usikivu wa rais katika kutekeleza maoni ya wafanyabiashara kuhusu mwenedo usiofaa wa mamlaka ya mapato na wizara husika.
0 Comments