Rais Dkt. Samia atema cheche Mjini Mpanda mkoani Katavi

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wakulima kote nchini kwa kiwango cha uzalishaji wa chakula na kuifanya nchi kuwa na utoshelevu wa chakula unaozidi  asilimia 120.

 

Rais Dkt. Samia ametoa pongezi hizo leo wakati akihutubia katika kilele cha Wiki ya Wazazi pamoja na mkutano wa hadhara iliyofanyika katika viwanja vya Azimio, Mpanda mjini. 

 

Aidha, Rais Dkt. Samia amesema utoshelevu huo umesaidia nchi kudhibiti mfumuko wa bei ambao umebaki asilimiia 3 na hivyo kuwaepusha wananchi na ugumu wa maisha unaotokana na uhaba wa chakula na mfumuko wa bei.

 

Rais DktSamia amezitaka Halmashauri zote katika mkoa waKatavi kuacha tabia ya kuwatoza wananchi ushuru wa mazao kwa kiasi kisichozidi tani moja na kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali hapo awali

 

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amesema Serikali ipombioni kukamilisha miradi ya umeme itakayoiunganisha Mikoaya Katavi na Kigoma kwenye Gridi ya Taifa ifikapo Oktoba 2024 na hivyo kuwa na umeme wa uhakika.


Rais Dkt. Samia SUluhu Hassan akisalimiana na Wazee Mjini Mpanda katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Katavi

Awali asubuhiRais Dkt. Samia alikagua mradi wa kupokeakupoza na kusambaza umeme wa Inyonga ambao ni sehemu yamradi wa ujenzi wa vituo vitatu vya Ipole (Sikonge), Inyonga(Mlele) na Mpanda wenye thamani ya shilingi bilioni 48. 

 

Mradi huu unaenda sambamba na mradi wa ujenzi wa njia yakusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi wenye thamani yashilingi bilioni 116.29 unaotarajia kukamilika ifikapo mweziOktoba mwaka huu.

 

Rais DktSamia pia amesema Serikali inaendelea kuifunguaKatavi kiuchumi kupitia miundombinu ya usafirishaji ikiwemoujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda na Bandari ya Karema ambayo italeta fursa za kibiashara na ajirakwa wananchi

 

 

Mwandishi: Sharifa Nyanga

Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments