Na. Shukuruimana Revokatus
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Philip Mpango awataka Mamlaka
ya Usafiri Aridhini LATRA watoe elimu kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto.
Dkt.
Mpango amesema hayo leo wakati wa kuzungukia mabanda yaliyojengwa katika uwanja
wa jamhuri wakati wa maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani
yanayofaniyika kitaifa jijini Dodoma.
Ameagiza Madereva wa magari, pikipiki Bajaji na
vyombo vingine vya moto wapewe elimu ya kutosha kwa lengo la kuondoa kabisa
ajari na vifo vinavyo sababishwa na ajari za barabarani nchini kote.
Dkt.
Mpango amesema Madereva wanaoendesha gari za Serikali wanaendesha kwa kasi
kubwa sana bila kujali foleni iliyopo barabarani hivyo LATRA wachukuwe hatua ya
kisheria na kutoa mafunzo kwa madeleva hao ili wafuate sheria na
kanuni za barabarani.
Ajali
zimekuwa nyingi kwasababu ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto kutopata
elimu inayowaongoza ili kuokoa maisha ya watanzania dhidi ya vifo vinavyotokana
na ajari za barabarani
Ameongeza
kwa kuwapa pongezi Polisi wanao husika na usalama barabarani kwa kuhakikisha
mifumo itakayo fanya kazi ili kusaidia kujua madereva wanaoendesha vyombo hivyo
kwa kutofuata sheria za kitaifa.
Mkuu
wa jeshi la polisi IGP Wambura anasema kutakuwapo na vifaa vinavyofanya ukaguzi
wa magari hapa nchi ili kutokomea ajari za barabarani.
Mapambano
dhidi ya ajari barabarani nila kutambuwa na nijukumu letu sote kwani kila mtu
anao wajibu wa kutimiza.
Watu
leo wamekusanyika na wadau mbalimbali wamekusanyika kwaajili ya kutoa nguvu na
kutoa elimu juu ya matumuzi sahihi ya barabara kwa kuhakikisha ajari
zinapunguwa na kuisha kabisa.
Jeshi
lapolisi wanaendelea kufuata maelekezo ya Serikali kuhusu mifumo ya
kielekituroniK ya udereva.
0 Comments