Naibu waziri wa ujenzi mhandisi Godfrey Kasekenya amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Rocktronic LTD anayejenga daraja la Itembe,Wilayani meatu mkoani Simiyu kukamilisha daraja hilo kabla ya msimu wa mvua kuanza .
Mhandisi Kasekenya
ametoa maagizo hayo jana
alipotembelea eneo la ujenzi wa daraja hilo
na kuridhishwa na mwenendo wa ujenzi unaofanywa na mkaandarasi mzawa.
“Jitahidi kuhakikisha ujenzi wa daraja hili
unakamailika kwa wakati kabla ya msimu wa masika kuanza ili kuwe na uwezekano
wa wananchi kupita katika daraja hili maana lisipokamilika tutakuwa tunarudi
kulekule tulikotoka “
Mheshimiwa Kasekenya ametoa agizo hilo kufuatia jamii ya
eneo hilo kulalamika kuwa wanaishi katika mazingira magumu kutokana na miundominu
mibovu inayounganisha mkoa wa Arusha na Simiyu.
Gregory Msaki ni mkazi wa Arusha na John Joseph mkazi
wa Bukundi Wilayani meatu wamesema kulikuwa na adha kubwa katika
barabara hiyo na iliwalazimu kukaa siku 3
au zaidi bila kupita eneo hilo wakati wa msimu wa mvua jambo liloathiri
maisha yao kijamii na kiuchumi.
Meneja wa Tanroads mkoa wa Simiyu Mhandisi Boniface
Mkumbo akitoa taarifa ya ujenzi amesema daraja hilo lina urefu wa mita 150 na
milango sita ya kupitisha maji na tayari ujenzi wake umefikia asilima 80.
Mkandarasi wa kampuni ya Rocktronic LTD David Sanagala
amesema changamoto inayosababisha kuchelewa kwa ujenzi ni kutokana na
kucheleweshwa kwa kwa malipo serikalini.
Sanagala anaeleza kuwa anadai zaidi ya shilingi
bilioni 2 na ameiomba serikali kulipa fedha hizo ili waweze kuendana na kasi ya
serikali .
Serikali inatekeleza ujenzi wa daraja hilo kwa gharama ya shilingi bilioni 8.4 na kukamilika kwake kutarahisisha shughuli za kiuchaumi kwa mikoa ya Manyara, Simiyu, Arusha na Singida.
Mwandishi: Shukuruimana Revokatus
0 Comments