Na. Shukuruimana Revokatus
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emanuely Nchimbi amempongeza Mbunge
wa jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako kwa kusimamia utekelezaji wa
miradi ya maendeleo kutokana na fedha zinazotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu
Hassan.
Balozi Nchimbi ametoa Pongezi hizo wakati
akihutubia wananchi na wana CCM katika uwanja wa Uhuru Kiganamo mjini Kasulu
akitaja kuwa Kasulu imebadilika hususani kwenye miondombinu na elimu na vituo
vya afya.
‘’Kwa
muda wa miaka mitatu maendeleo yamekuwa makubwa sana na tunatarajia baadhi ya
miundombinu ambayo haijakamilika inakamilika haraka sana ili kuendelea na mambo
mengine ya kuijenga nchi yetu” Amesisitiza Dkt Nchimbi
Katibu
mkuu wa CCM ametumia pia fursa hiyo kueleza kushangazwa kwake na namna rais
Samia Suluhu Hassan anavyoonesha uwezo mkubwa wa kuongoza taifa na kutekeleza
miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa na bwawa la Umeme la Mwalimu
Nyerere.
Dkt.
Nchimbi amebainisha kuwa baada kufariki kwa aliyekuwa mwasisi wa miradi
mikubwa, jamii haikutarajia kuona rais mwanamke akiongoza vema utekelezaji na
ukamilishaji wa miradi hiyo, lakini mama Samia ameonesha bila shaka kuwa
wanawake wanaweza.
“Akina
mama tembeeni kifua mbele, wanawake wanawaza na mama samia ameonesha mfano kuwa
mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa” amesisitiza Dkt Nchimbi
Awali,
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Zainab Katimba alitumia mkutano huo kuonya
wahudumu wa afya ya msingi kutotoza wananchi malipo ambayo hayajaidhinishwa na
serikali akiwataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi endapo watapata usumbufu
wowote.
“Nawaagiza
wakurugenzi fuatilieni na hakikisheni huduma za afya ya msingi zinatolewa kwa
jamii bila usumbufu wowote, na ninyi wananchi endapo mtakutana na vikwazo toeni
taarifa kwa mamlaka husika ili matatizo yatatuliwe haraka.
Naye
mmoja wa wananchi wilayani Kasulu Bi. Edina William amesema baadhi ya wahudumu
wa vituo vya afya wamekuwa wakitoa tozo kubwa sana kwa wauguzi pa bila kufuata
taratib za kituo husika na umekuwa niutaratibu ambao haujazoeleka ndani ya
jamii
‘’Wahudumu
wanaotoa huduma katika vituo vya afya waanapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu za vituo husika, serikari imetoa
maelekezo kulingana na umri wa mtu alio nao au rika tofauti kuhusu malipo yay a
huduma za afya msingi.
‘’Mfano
watoto kuanzia mwaka sifuri mpaka miaka mitano huduma zao ni bure lakini
unakuta motto wa umri huo anatolewa malipo kitende ambacho siyo kizuri kabisa
na mtu kama ana bima ya afya isiwe
sababu ya kumtoza pesa nyingine wakati amesha lipia’’ alisema William
Katibu
mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emanuel Nchimbi yupo mkoani Kigoma kwa ziara
ya kikazi na kusikiliza kero za wananchi.
0 Comments