Mwandishi wa habari aliyeshikiliwa nchini Burundii aachiwa huru

Mwandishi na mtangazaji wahabari Floriane IRANGABIYE amepewa msamaha na Raisi wa Burundi Evariste Ndayishimiye baada ya kushikiliwa na vyombo vya usalama akituhumiwa kukiuka taratibuu za kitaaluma.

Katika walaka ambao uliotolewa Jumatano ya tarehe 14 August 2024 Rais Ndayishimiye amefahamisha kuwa makosa ya mwandishi na mtangazaji Floriane IRANGABIYE amesamehewa makosa yake na kwamba ataachiliwa huru.

Mtangazaji huyo aliwekwa kiziwizini alipokuwa matembezini nchini Burundi akitokea nchini Rwanda ambapo anaishi na kufanyakazi ya utangazaji katika kituo cha radio cha IGICANIRO.

Floriane ametimiza miaka 2 akiwa gerezani ambapo alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 10. 

Kwa mjibu wa mahakama kuu ya Burundi mtangazaji huyo alikutwa na hatia kwa kosa la kuchochea uvunjifuu wa amani na kuhatarisha usalama wa nchi.

Katika miaka miwili aliyokaa gerezani Irangabiye amekuwa akihamisha magereza mbalimbali tangu alipokamatwa ambapo awali alifungwa kwenye gereza kuu la Bujumbura baade akahamishwa kwenye Gereza la mkoani Muyinga, na anaachiwa akiwa kwenye gereza la mkoani Bubanza.

Mashirika ya haki za binaadamu pamoja na waandishi wa habari mbalimbali wamekuwa wakilaani sana kufungwa kwa mtangazaji Floriane na kusisitiza kuachiliwa kwake.

Imeandikwa na. David NDEREYIMANA, Bujumbura

Post a Comment

0 Comments