Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Camillus Wambura amemuhamisha kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma (SACP) Theopista Mallya kwenda makao makuu ya polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) George Katabazi mbayae alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara.
Mabadiliko hayo yanakuja baada ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishina msaidizi wa polisi SACP Theopista Mallya kutoa taarifa yenye utata kwa vyombo vya habari Agust 18 ,2024 kuhusu sakata la msichana aliyebakwa akitaja kuwa “binti aliyebakwa na kulawitiwa alikuwa anajiuza”
Taarifa iliyotolewa mapema leo na msemaji mkuu wa Jeshi la Polisi David Misime mapema leo imesema, kauli iliyotolewa na aliyekuwa RPC Dodoma kamanda Mallya siyo msimamo wa Jeshi la Polisi
“Jeshi la polisi lingependa kutoa taarifa kwa kauli hiyo kama
inavyoonekana kwenye kichwa cha habari siyo msimamo wa jeshi la polisi na
kwamba kauli sahihi ya jeshi la polisi ni kama ilivyotolewa na msemaji wa jeshi
la polisi kwa umma Agosti 4,6,9, 2024 “
Msemaji wa Polisi David Misime ameweka bayana kuwa watuhumiwa wa Kesi hiyo wanafikishwa mahakamani leo Agosti 19 jijini Dodoma .
Kabla ya kuteuliwa kuwa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma machi 14, 2024 Kamshina msaidizi wa jeshi la polisi Theopista Mallya alikuwa kamanda wa mkoa wa Songwe na nafasi yake kuchukuliwa na Augustino Senga ambaye alikuwa mkuu wa jeshi la polisi Zanzibar
Kamanda Mallya amedumu katika nafsi hiyo kwa miezi mitano kabla ya kuondolewa mapema leo ambapo vyombo vya habari na wana harakati walifuatilia na kuandika kuhusu kauli yake yenye utata juu ya tukio la ubakaji.
Awali akifanya
mahojiano na Gazeti la Mwananchi,Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima aliwataka wananchi kuwa watulivu kuhusu mwenendo wa upelelezi washitakiwa wa kesi hiyo akitaja kuwa haki itatendeka .
“Ndugu wananchi nimepokea hisia zenu ,maoni na maswali yenu ,amabayo mmeelekeza kwangu nimewasiliana na mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani tayari nae amepokea na anafanyia kazi hivyo tumpe nafasi atatoa taarifa yake"
Waziri Gwajima alisisitiza kuwa sheria itachua mkondo
wake “Nawasihi tujipe muda wa kuaamini kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa
sharia na itaonekana bayana na si vinginevyo “
Video ya tukio
hilo la kikatili kwa binti aliyedai ni
mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Agosti 4, 2024, Ikimuonyesha binti
huyo akibakwa na kuingiliwa
kinyume na maumbile na vijana 5 waliodai
kutumwa na afande mmoja (hajatajwa) kufanya tukio hilo kutokana na kuwa na mahusiano na mume wake
.
Mwandishi: Hariath Kamgisha
0 Comments