Wanawake Ukonga wanolewa kupinga Rushwa ya ngono

Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Kipunguni, Ukonga Dar es Salaam, Selemani Bishagazi amewafunda wanawake kuelekea katika chaguzi nchini.

Hamasa hiyo imetolewa leo wakati wa mafunzo kwa wanawake wa jimbo la Ukonga kama sehemu ya mpango wa elimu ya uraia na uchaguzi wakati taifa likijiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu Miongoni mwa mada katika mafunzo kwa wanawake hao ambayo yameandaliwa na Sauti ya Jamii Kipunguni leo ni pamoja na namna ya kupambana na rushwa ya ngono katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi nchini. Bishagazi amewata kutumianhaki yao vizuri kwenye chaguzi hizo ikiwamo kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura watakapofikiwa katika maeneo yao. Amesema bado kunahitajika nguvu ya ziada katika kutoa elimu ya namna ya kupambana na kuishinda rushwa ya ngono hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka kesho. "Nilichogundua ni kwamba bado wapo baadhi ya watu ambao wanaendelea kutesa wengine kupitia rushwa ya ngono na waathirika wakubwa ni wanawake, baadhi yao wanashindwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwa sababu wanakumbana na vizingiti vya kuomba rushwa hiyo,"amesema Bishagazi.


Post a Comment

0 Comments