Serikali ya Iran imewakamata watu 12 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Israel,huku kikosi cha mapinduzi cha Iran kimesema watu hao walikuwa wanashirikiana na Israel kupanga njama ya kuvuruga usalama wa Iran.
Taarifa iliyotolewa na VOA Septemba 22,2024 kuwa kikosi hicho cha Iran kimebainisha kwamba majasusi hao 12 walikamatwa katika mikoa sita tofauti,nchini humo licha ya kutotaja siku waliyokamatwa.
"Wakati utawala wa Kizayuni na washirika wao wa nchi za
Magharibi, hasa Marekani wameshindwa kufanikiwa katika mpango wao mabaya
dhidi ya wananchi wa Gaza na Lebanon, hivi sasa wanataka kuhamisha mzozo nchini
Iran kwa kupanga msururu wa njama dhidi ya usalama wa nchi yetu" taarifa ya
kikosi hicho ilisema.
Septemba 19 mwaka huu Israel olitoa ripoti ya kumkamata raia wake mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika njama na Iran ya kumuua Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wa idara za usalama za Israel
Hata hivyo hali ya taharuki huko Mashariki ya Kati
imeongezeka tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa
Hamas huko Gaza, ambao ulitokana na kundi la Hamas kuishambulia kwa makombora
Israel mwaka mmoja uliyopita na Hivi
sasa mgogoro huo umeendelea mpaka nchini
Lebanon na kundi la wanachama wa Hezbollah.
Mwandishi; Harieth Dominick
Mhariri; Sharifat Shinji
0 Comments