Afrika (CDC) yaonya mataifa ya Magharibi kuhusu Mpox.


Dkt. Jean Kaseya mkurugenzi mkuu wa (CDC). (Picha:Mulugeta Ayene/Ap/ Picture alliance)

Mkuugenzi  mkuu  wa  Taasisi ya kuzuwia na kupambana na magonjwa wa Umoja wa Afrika (CDC) Dkt. Jean Kaseya amesema ni wakati kwa nchi za Magharibi kuonyesha kuwa zimejifunza kutokana na janga la Uviko-19 na sio kuitelekeza Afrika wakati wa mlipuko wa Homa ya Nyani. 

Ameyabainisha hayo Septemba 12, 2024 huku akisema vifo vipya 107 na visa vipya 3,160 vya ugonjwa huo vilirekodiwa wiki iliyopita  ikiwa ni wiki moja baada ya shirika la Afya Duniani (WHO) kuzindua mpango wa kukabiliana na Janga hilo.

Aljazeera imechapisha kuwa, kituo cha kuzuwia na kupambana na magonjwa cha Umoja wa Afrika (CDC), kimesema kina ungufu wa dola milioni 600 za  kukabiliana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa umesambaa katika mataifa 14 Barani Afrika.

Mpox ilitangazwa kuwa dharura ya kimataifa mwezi Agosti na Shirika la Afya Duniani (WHO), kufatia ongezeko la  visa vya aina mpya ya Kirusi cha ugonjwa huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kitovu cha mlipuko huo.

Shehena ya chanjo ya Mpox ikiwasili jijini Kinshasa, Septemba mwaka huu.

Kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya DRC, kumekuwa na karibu kesi 22,000 na vifo 716 vinavyohusishwa na virusi hivyo vilivyorekodiwa tangu Januari mwaka huu.

Hadi sasa, karibu dozi 200,000 za chanjo zimewasilishwa DRC na Umoja wa Ulaya, pamoja na nyingine takriban 50,000 kutoka Marekani huku  ikiwa  Japani imeahidi kutoa dozi milioni 3 na laki 5 za chanjo ambayo inaweza kutolewa kwa watoto, ambaoni miongoni mwa wahanga wakuu wa janga hilo.

Mwandishi; Abel Mahenge


Post a Comment

0 Comments