Afrika Mashariki yazinduza Jukwaa la Mboga na Matunda.

Jukwaa  maalum la kikanda la kukuza sekta ya mboga na matunda (horticulture)katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika(COMESA) limezinduliwa rasmi kwa lengo la kuhakikisha mazao ya viazi mviringo,vitunguu na Parachichi yanapata soko zaidi Afrika na nje ya bara hilo.

Ufunguzi huo umefanyika Septemba 15, 2024 chini ya  Mkurugenzi wa Taasisi ,TAHA nchini, Dk, Jacqueline Mkindi na Mtendaji Mkuu wa Shirika la COMESA /ACTESA, Dk John Mukuka jijini Arusha na kushuhudiwa na wakulima kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Dk Mkindi amesema uanzishwaji wa jukwaa hilo utawezesha wadàu wa tansia ya ‘horticulture’ kikanda kuandaa mpango wa pamoja wa kutatua changamoto za kisekta ikiwemo uwepo wa ushirika wa kibiashara na nchi za Umoja wa Ulaya.

Aidha ameongeza kuwa utiaji saini wa mkataba wa jukwaa hilo unatoa fursa ya kupeleka mazao ya Parachichi,Viazi mviringo huku akitaja zao la parachichi kukua zaidi ikiwemo wakulima kunufaika na kilimo kutokana na mazao wayanyozalisha.

Kilimo cha mboga na matunda kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 30  Hapa Tanzania huku, hali ya hewa ikiruhusu ustawi wa aina mbalimbali za mboga na matunda, na uzalishaji wake unakadiriwa kuwa zaidi ya tani 2,750,000 kwa mwaka .

Mboga na matunda ni muhimu  kwa afya ya binadamu kwani zinatoa vitamini, madini, na nyuzinyuzi zinazohitajika mwilini kila siku  Pia, zinasaidia katika kupambana na magonjwa sugu, kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili, na kuboresha Afya ya ngozi na nywele .

Takwimu zilizochapiswa mwaka 2023 zilionesha kuwa tani 26,826.3, ziliingiza mapato ya takriban dola million 73 kutoka nje ya nchi huku makadirio ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa yakiaonesha kuwa ifikapo mwaka wa 2033, uzalishaji wa parachichi wa Tanzania unatarajiwa kuongezeka hadi tani 393,669, na mauzo ya nje yanatarajiwa kufikia tani 236,201.5, na kuleta mapato ya dola milioni 449 kwa mwaka kama bei itabaki kama ilivyo.

Mwandishi; Abel mahenge

Post a Comment

0 Comments