Aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanga wa kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania (KKKT) Chediel Elinaza Sendoro amefariki dunia usiku wa jumatatu ya septemba 9,2024 kwa ajali ya gari iliyotokea Eneo la Kisangiro wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro .
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa Kanisa la KKKT askofu Dkt Alex Malasusa amesema ajali hiyo imehusisha gari la marehemu Askofo Sendoro ambalo liligongana na lori wakati askofu alipokuwa akielekea nyumbani kwake usiku .
Katika ajali hiyo marehemu alikuwa na mtoto wake ambae amenusurika na anaendelea na matibabu .
"Nawaombea faraja kwa neno kutoka katika Biblia takatifu kitabu cha Waebrania 13:14 "maana hapa hatuna mji udumuo bali twautafuta ule ujao mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi"
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa,akiongea na mwananchi amesema ajali hiyo ilitokea 1:30 usiku siku septemba 9,2024 , Wakati gari lilokuwa likiendeshwa na Askofu huyo likitokea barababara ya Himo - Mwanga kuyapita magari mengine na kugongana uso kwa uso na Lori .
"Ni kweli leo saa 1: 30 imetokea ajali na Askofu wa Sendoro amefariki dunia eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga , ambapo gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na Askofu lilipata ajali na kusababisha kifo chake " alisema Kamanda "
Aidha Kamanda Maigwa amesema Chanzo cha ajali bado kinaendelea kuchunguzwa na mwili wa marehemu tayari umechukuliwa kutoka eneo la tukio.
Askofu Chediel Sendoro, ndiye askofu wa kwanza kuongoza Dayosisi ya Mwanga aliingizwa kazi Novemba 6,2016 baada ya Dayosisi hiyo mpya kuzaliwa kutokana na kugawanywa kutoka dayosisi mama ya Pare .
Mwandishi : Harieth Kamugisha
0 Comments