Antonio Guterres alaani mauaji ya wafanyakazi wake Gaza.


   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amepinga na kulaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina.

Kauli hiyo ameitoa September 12, 2024 kupitia mtandao wa x zamani kama twiter baada ya shambulizi lilifanywa na Israel siku ya Jumatano na kusema kuwa shambulio hilo linakwenda kinyume na sheria ya umoja wa mataifa.

Awali siku ya Alhamisi Jeshi la Israel (IDF) lilikiri na kuthibitisha kuhusika na mashambulizi hayo huku likisema lilifanya shambulio sahihi dhidi ya magaidi waliokuwa ndani ya kituo cha kamandi ya Hamas.

Kwa upande wa Jeshi la Hamas limekanusha kutumia maeneo ya shule, hospitali na maeneo mengine ya umma kwa matumizi ya kijeshi.

Kwa mujibu wa Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina limesema kuwa shambulio hilo ni tano katika shule hiyo tangu kuanza kwa vita hiyo mwezi October, 2023 huku ikiwa na idadi kubwa ya watu waliofariki ukilishanisha na mashambulizi yaliopita.

Kwa upande mwingine VOA  imeripoti kuwa Jumla Wapalestina 20, wakiwemo wanawake watano na watoto watano, na makamanda watatu wakuu wa kundi la Islamic Jihad na washambuliaji wanne waliuawa tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya kabla ya alfajiri siku ya Jumanne, maafisa wa afya wa Palestina wamesema.

Mwandishi; Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments