Bashe afungua maghala ya chakula kwa wakulima.

Waziri wa kilimo nchini Husein Bashe amewataka wananchini na wakulima wote nchini kukusanya mazao yao katika maghala madogo yaliyoko katika maeneo yao ili kupunguza gharama za ufanyaji wa biashara za mazao ya chakula na kulipa kwa wakati.

Amesema hayo leo September 5, 2024 jijini Dodoma katika Bunge la 12 mkutano wa sita kikao cha nane wakati akijibu swali la mbunge wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Festo Richard  Sanga lililohaoji ni lini wizara itasimamia wakulima ambao hawajalipwa stahiki zao kwa wakati.

Aidha waziri Bashe ameongeza kuwa wizara ya kilimo imetoa wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka sekta ya viwanda na biashara pamoja na wizara ya fedha kuandaa na kujenga mghala ya kuhifadhi mazao ya wakulima.

Kwa upande mwingine bashe wamesema kuwa serikali imeandaa mpango wa wakulima kutumia manghala ya kuhifanyi chakula kutumika kama vituo vya mauzo ili kupunguza changamoto ya kutolipwa kwa wakati.

Waziri Bashe ametoa maagizo hayo kulingana na muendelezo wa mlimbikizo wa madeni ya wakulima kwa wafanyabiashara wa mazao na kutokawa na bei maalumu ya mazao hasa mazao ya chakula.

Kwa mujibu wa chapisho la Juni 2024 la wizara ya fedha,  Mwaka 2023, mchango wa shughuli za kilimo katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 26.5 ikilinganishwa na asilimia 26.2 mwaka 2022. huku, shughuli ndogo za mazao zilichangia asilimia 16.1 katika Pato la Taifa, 

  Mwandishi; Ramadhani zaidy

Post a Comment

0 Comments