Kiwanda cha sukari cha SOSUMO nchini Burundi kimetangaza ongezeko la bei ya sukari
kutoka 3300 faranga ya Burundi hadi kufikia 8000 kwa kilo moja ya sukari ,bei hiyo
imetangazwa rasmi siku ya septemba 15 ,2024 na kiwanda hicho .
Akieleza sababu zilizopelekea kupanda kwa bei ya sukari Aloys
Ndayikengurukiye Kiongozi wa kiwanda cha sukari SOSUMO amesema kupanda kwa bei
ya sukari kunatokana na changamoto ya upatikanaji malighafi pamoja na vifaa vya
mitambo ya uendeshaji kupanda bei katika soko la kimataifa.
Hii ni baadhi ya mifuko ya sukari inayozalishwa na kiwanda cha SOSUMO
kilichotangaza kupandisha bei ya Sukari nchini Burundi .
Katika hatua nyingine ,Wananchi wameonesha kusikitishwa na kupanda kwa bei ya sukari
wakisema kuwa imepandishwa zaidi ya marambili ikilinanishwa na bei ya awali
,Ikizingatiwa na ugumu wa maisha uliopo , hivyo wameiomba serikali nchini humo
kufanya tathimini ya bei hiyo na kupunguza bei ya sukari .
Hivi Karibuni Serikari ya Burundi ilikuwa imeruhusu wafanyabiashara kuingiza sukari
kutoka nje ya burundi,Kutokana na kiwanda hicho kilichopo mkoani Rutana kusini mwa
Burundi kutoweza kukidhi mahitaji ya sukari kwa raia wa Burundi.
Mwandishi: David Ndereyimana.
0 Comments