Biden alaani jaribio la pili la mauaji ya Trump

Rais wa Marekani, Joe Biden, amelaani  jaribio la pili la mauaji dhidi ya mtangulizi wake, na kukemea ghasia za kisiasa kuwa sio tabia za Marekani. 

Rais Biden amesema hayo septemba 16 ,2024  katika mkutano wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vya watu weusi (HBCU ) jimboni Philadelphia  na kusisitiza kuwa Marekani ni nchi ya Demokrasia .

“Hakuna mahali kwa kufanya vurugu za kisiasa Marekani Kuna usuluhishi wa tofauti zetu ,” alisema  Biden 

Amesema tofauti za wamarekani zinasuluhishwa Kwa  amani  kupitia sanduku la kura, sio kwa mtutu wa bunduki. Aidha amesisitiza kwamba Marekani inateseka mara nyingi na mikasa ya mauaji ya bunduki na kwamba njia hiyo haisuluhishi chochote zaidi ya kusambaratisha nchi.

Maoni ya Biden yametolewa takriban saa 24 baada ya maafisa wa idara ya ulinzi wa viongozi ya Marekani, kumwona Mtu mwenye bunduki aliyejificha kwa takriban saa 12 vichakani kwenye uwanja wa gofu wa Rais mstaafu   Donald Trump West Palm Beach Florida likiwa ni jaribio la pili la kumuua rais huyo mstaafu.

MwandishiHarieth Dominick

Post a Comment

0 Comments