Biden: Sudani yahitaji Uhuru,Amani na Haki.


Picha; DW                                                                                        

Rais wa Marekani Joe Biden septemba 17,2024 amezitolea wito pande zinazozozana nchini Sudan kushiriki tena kwenye mazungumzo ya amani.

Rais wa Marekani Joe Biden ameziomba pande hizo zinazopigana nchini sudan kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao na kurudisha vikosi vyao nyuma ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji bila vikwazo.

Aidha ameelezea wasiwasi wake juu ya mji wa El-Fasher, moja ya miji mikuu mitano ya jimbo la Darfur, ambao umezingirwa na wanamgambo wa RSF tangu mwezi Mei ambapo Mji huo unakaliwa na wakazi karibu milioni 2 waliokimbia makazi yao


Kutokana na mapigano hayo ameongeza kuwa Marekani haitaacha kujitoa kwa ajili ya watu wa Sudan wanaostahili kuwa na uhuru, amani na haki.

Vita vya Sudan vilianza mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya jeshi la Sudan na RSF, na tayari vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine kuyakimbia makazi yao.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa.

Mhariri; Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments