Kiongozi wa upinzani nchini Uganda kupitia chama cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu kama (Bobi Wine) amejeruhiwa mguuni na bomu na kilipuzi chenye kutoa machozi wakati wa makabiliano na Jeshi la Police nchini humo.
Tukio
hilo limetokea wakati kiongozi huyo alipokuwa njiani akisafiri kuonana na
mawakili wake siku ya jumanne katika eneo la Buhindo takribani kilometa 20
kaskazini mwa mji mkuu wa nchini hiyo Kampala.
Jeshi
la polisi nchini humo limetoa taarifa kuwa maafisa wa eneo hilo waliripoti kuwa
kiongozi huyo alijijeruhi mwenyewe wakati akiingia kwenye gari lake.
Aidha
kwa upande wa wataalamu wa afya katika hospitali ya Nsambya mjini Kampala
wakati wakizungumza na waandishi wa habari wamesema kuwa wanatarajia kufanya
matibabu ya upasuaji ya kuongdoa vipande vya bomu hilo.
Ikiripoti DW kuwa Bobi Wine atafanyiwa upasuaji, siku moja baada ya kujeruhiwa mguu katika tukio la vurugu ambapo chama chake jana kiliripoti kwamba alijeruhiwa kwa Bomu la machozi.
Wakili wa mwanasiasa huyo, George Musisi amefahamisha kwamba hivi sasa hayuko katika hali mbaya ingawa kwa mujibu wa madaktari atafanyiwa upasuaji kuondowa vipande vya bomu la kutowa machozi lililompiga mguuni.
Imeandikwa na: Ramadhan Zaidy
0 Comments