Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema haiwezekani kulihukumu jeshi la polisi kwa baadhi ya polisi wachache wanaofanya makosa kinyume cha sheria.
Dkt Nchimbi amsema hayo leo septembe 13,2024 wakati akitoa msimamo wa chama cha mapinduzi mbele ya wahariri pamoja na waandishi wa habari waandamizi katika ukumbi mdogo wa CCM, jijini Dar es salaam, na kusisitiza kuwa jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wawanchi na mali zao.
Aidha Dkt .Emmanuel Nchimbi amsema Tangu mwaka 2017 hadi 2023 polisi 42 wameuawa na 141 wamejeruhiwa kutokana na kazi ya kuhakikisha wanasimamia usalama wa wananchi pamoja na malizao.
"Hatuwezi kulaumu jeshi zima la polisi kwa makosa ya polisi wachache hivi juzi kulikuwa na mtu alijifanya ni mwandishi wa habari aliyekuwa anapita katika taasisi za serikali akitaka pesa kwa madai ya kuandika makala za CCM lakini nilipomuangalia usoni wala sio mwandishi wa habari ni tapeli, sasa siwezi kuwalaumu waandishi wote wa habari ni mtu mmoja" amesema Dkt .Nchimbi.
Katika hatua Nyingine Dkt . Nchimbi amesema ameamua kuzungumza na jamii kutokana na hofu na sintofahamu ya utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia na kwamba CCM inalaani na haiungi mkono yanayoendelea nchini.
"Hakuna chama chochote dunia kinacho weza kuunga mkono wananchi wake kutekwa na kuuwa kwasababu watakinyima kura kwahiyo tuache maneno ya uchochezi ,CCM hatuungi mkono viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani"
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa viongozi wa chama cha Dokrasia na maendeleo CHADEMA Mbowe na Mnyika hawahusiki na utekaji na kuuwawa aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti ya chama hicho badala yake uchunguzi ufanyike haraka ili kubaini wahusika na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria .
Alipoulizwa na mwandishi wa habari ikiwa chama chake kitaruhusu wachunguzi kutoka nje ya nchi kuchunguza tukio la kifo cha Kibao ,Dkt Nchimbi amesema kuwa kazi ya uchunguzi ni wajibu wa serikali ila kama serikali itataka usaidizi kutoka nje, chama cha mapinduzi kikotayari kutoa ushirikiano.
Katibu wa CCM amesema hayo wakati kukiwa na vuguvugu la wananchi ,vyombo vyahabari na makundi ya haki za binadamu yakitaka serikali kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini waliyohusika na kifo cha Ali Kibao wa CHADEMA.
Ali Mohamed Kibao alitekwa tarehe 6 septemba 2024 na watu wenye silaha waliosadikiwa kuwa polisi, Eneo la kibo Coplex Tegeta jijini Dar es salaam akiwa kwenye basi la Tashrif akielekea nyumbani kwake Jijini Tanga na baada ya siku moja mwili wake ulikutwa eneo la Ununio akiwa amepoteza maisha .
Mwandishi: Harieth Kamugisha.
0 Comments