Dkt. Dotto Biteko aipongeza Banki ya NMB

Banki ya NMB imekabidhi Hundi ya Shilingi milioni 50 kwa Naibu Waziri Mkuu NA Waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Wavulana ya Bunge  Wakati wa Bonanza la Bunge, NMB pamoja na wadau wengine.

kwa mujibu wa Theguardian makabidhiano hayo yamefanyika  leo Septemba 04, 2024  katika viwanja vya shule ya sekondari John Merlin Jijini Dodoma huku Biteko akielezea kuwa msada huo utaimarisha juhudi za wabunge katika ujenzi wa shule hiyo baada ya kukamilika shule ya Wasichana Bunge.

Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Juma Kimori amezungumza kuwa  Benki hiyo itaendelea kuonesha mchango wake kwa jamii ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita na mipango mbbalimbali inayoendeshwa na Wabunge.

Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson akizungumza katika hafla hiyo amesisitiza haja ya kuendelea kushirikiana na benki hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali sambamba na kuhamasisha matumizi sahihi ya huduma za kibenki katika ngazi zote za jamii ikiwemo vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Mhe. Festo Sanga amesema mbali na kudhamini Bonanza hilo, lakini NMB wameonyesha ushindani mkubwa hata kuishinda Timu ngumu ya Bunge ya Mpira wa Miguu kwa magoli 3-0.

Bank ya NMB, imekuwa na utamaduni wa kuunga juhudi za serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyofanya mwaka 2016 kwa kukabidhi msaada wa madawati, vitanda na Magodoro katika shule ya sekondary Namwai iliyopo Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.


Mwandishi; Ellukagha Kyusa


Post a Comment

0 Comments