Rais Dkt. Samia atoa agizo kifo cha kada wa CHADEMA.

Rais wa Jamhuri ya Mumgano wa Tanzania  Dkt. Samia.

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameamuru vyombo vya usalama nchini kufanya uchunguzi wa matukio ya utekaji nyara na mauaji yanayoendelea nchini humo.

Rais Samia ametoa agizo hilo usiku wa kuamkia September 9, 2024 baada ya kifo cha aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ali Mohamed Kibao na kusema kuwa Tanzania inaongozwa na serikali ya kidemokrasia.

"Kwanza natoa pole kwa familia ya Kibao na wanachama  wote wa CHADEMA, pia naagiza vyombo vya ulinzi kuniletea taarifa za kina kuhusu tukio hili baya  matukio mengine ya namna hii  kwa haraka maana nchi yetu ni ya Kidemokrasia kila ria ana haki ya kuishi"

Kwa upande wa msemaji wa jeshi la Polisi, David Misime akizungumza na MWANANCHI, amesema wanafatilio tukio hilo kwa kina na wameongeza nguvu kutoka makao makuu.

"Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi mkali kutoka na timu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai imetumwa kuongeza nguvu"

Awali mwenyekiti wa chama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mboye ametoa rai kwa vyombo vya usalama nchini kufanya uchunguzi wa kifo cha Kibao huku akisisitiza wahusika kufikishwa katika vyombo vya kisheria.

Mwili wa aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ali Kibao ulikutwa siku ya jumapili nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam ukiwa na mjeraha ya kipigo na tindikali usoni.

Taarifa zinaeleza kuwa Ali Kibao alitekwa nyara siku ya ijumaa na watu waliodhaaniwa kuwa ni maafisa wa polisi akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea mji wa tanga ulioko kaskazini mwa Tanzania.

Mwandishi; Shukuruimana Revokatus

Post a Comment

0 Comments