Umoja wa ulaya (EU) umetangaza kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Iran kutokana na uamuzi wake wa kuipatia Moscow makombora ya masafa marefu
Msemaji wa EU Peter Stano amesema hayo usiku wa
kuamkia September 10, 2024 , kuwa viongozi wa Brussels wanaendelea
kuzifuatilia kwa kina taarifa hizo na iwapo zitathibitika watachukua uamuzi wa
kuidhuru Iran juu ya uamuzi wao.
Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran, Nasser Kanani amekanusha vikali taarifa hizo na kudai kuwa Iran haiwezi kuegemea upande mmoja wa vita vinavyo endelea kati ya Urusi na Ukreine .
Awali vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa Marekani inaamini Iran inapeleka silaha Urusi za kutumia kwenye vita dhidi ya Ukraine.
Kwa upande mwingine ,Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Urusi Dmitry Peskov alikanusha kuhusiana na taarifa hizo na kusema si za kweli , wakati alipoulizwa na jarida la Wall Street nchini Marekani .
Iran na Urusi wamekuwa washirika wa karibu katika nyanja mbalimbali ikiwemo ,kijeshi ,kibiashara na uchumi tangu wakati wa vita nchini Syria .
Mwandishi: Ramadhani Zaidy
0 Comments