Fabrice Ngoma, Mzamiru Yasini Matatani.

Wakati klabu ya Simba ikiendelea kujiimarisha katika maeneo tofauti ili kuijenga timu yenye ushindani mkubwa kitaifa na kimataifa Mwalimu Fadlu Davis amewapa mtihani mzito baadhi ya wachezaji wanaocheza nafasi moja hususani katika eneo la kiungo. 

Hili linajiri baada ya Mchezaji Fernandez Mavambo kuweza kuonesha uwezo mzuri katika eneo la kiungo na kucheza kwa nidhamu,huku Fabrice Luamba Ngoma na Mzamiru Yasini "kiungo punda" wakiwa na historia ya kufanya vizuri katika michuano mbalimbali hususani ya kimataifa. 

Simba SC wanajiandaa kwa michezo ya kimataifa kombe la shirikisho barani Africa ambapo miamba hiyo ya soka nchini Tanzania wanatarajia kurusha karata yao ya kwanza ugenini dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libiya siku ya jumapili September 15 saa 20:00 usiku huku mchezo wao wa marejeano ukitarajiwaa kupigwa September 20.

Hata hivyo Simba SC kabla ya mchezo huo wa kimataifa wantarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya  Maafande wa JKT Tanzania siku ya juma mosi ya tarehe Septemba 07/2024 katika Uwanja wa KMC Complex majira ya saa 10:00 jioni.

Miamba hiyo ya soka yenye makazi yake jijini Dar es Salaam iliozaliwa 1936 imekuwa na mafanikio mazuri katika ngazi ya kimataifa ambapo msimu wa 2023/2024 ilishiriki klabu bingwa Afrika nakuishia katika hatua ya robo fainali huku msimu huu wa 2024/2025 ikishiki kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni mara ya saba[7].

Mwandishi; Eunice Jacob

Post a Comment

0 Comments