Urusi yaendeleza mashambulizi Kharkiv.

Gavana wa mji mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine, Oleh Syniehubov amesema kuwa majengo 18 na watu takribani 20 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na Urusi usiku wa kuamkia Septemba 23, 2024.

Kwa mujibu wa Gavana huyo amesema kuwa Urusi imefanya mashambulizi mapya kwenye mji huo huku akisema kuwa wakazi wa kadhaa wa majengo yalioharibiwa na shambulizi hilo wamelazimika kuhamishiwa maeneo mengine.

DW imeripoti kuwa, awali Septemba 21, 2024 Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisaini sheria mpya ya ongezeko la karibu dola bilioni 12 kwa matumizi ya jeshi la nchi hiyo ili kuongeza mapambano katika vita vyake na Urusi.

Mbali na ongezeko la fedha hiyo Rais Zelensky ameomba nchi za magharibi kutuma silaha zaidi ili kuisaidia Ukraine pamoja na kulinda raia wa nchi hiyo katika vita dhidi ya Urusi.

Kharkiv ndio mkoa wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine huku ukiwa na idadi ya watu takribani milioni 1.4 ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake mwaka 2022.

Mwandishi; Ramadhan Zaidy

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments